NDOA

NDOA
Ndoa ni taasisi ambayo iliasisiwa na Allah ‘Azza wa Jallah
Mwenyewe pale alipowaunganisha baba yetu Adam na mama yetu Hawa kuishi pamoja kama mume na mke.

Kwa hiyo, Uislamu kama dini na mfumo wa maisha, umeweka kanuni, sheria na hukumu za kufuatwa ndani ya taasisi hii tukufu (ya ndoa).
Tutakusanya mafundisho yote muhimu yenye kuhusu taasisi hii kutoka katika vyanzo vikubwa na chimbuko la sheria na mafundisho ya Uislamu, ambavyo ni Qur’ani na
Sunnah. Nitazileta kwenu ili zimnufaishe kila mtumiaji wa mtandao katika maisha yake ya ndoa.

Ndoa nyingi zimekuwa zikilegalega na hatimaye kufikia ukomo (talaka) kwa sababu ya wanandoa kuingia katika taasisi hii bila kufanya maandalizi ya kutosha. Kwa hakika kama ambavyo kila kazi inahitaji mtu awe na ujuzi wa kazi hiyo, ndivyo hivyo hivyo ndoa inahitaji ujuzi wa namna ya kuishi na mwenza na pia namna ya kulea watoto watakao patikana kutokana na ndoa hiyo

Comments