NI UPUUZI KUMHUSISHA ABDULLAH BIN SABA’ NA MASHI’A

NI UPUUZI KUMHUSISHA ABDULLAH BIN SABA’ NA MASHI’A
Katika masahaba na tabiin hapakuwepo na mtu anayeitwa Abdullah Ibn Saba, huu ulikuwa ni ubunifu wa mtu aliyekuwa akiitwa Seif.

Ukweli huu umetokana na utafiti uliofanywa na mwanachuoni
mtafiti, Al-Askari. Soma kitabu chake: “Abdallah bin Saba’ na ngano nyinginezo

Kwa kweli Waislamu wa Madhehebu ya Shia kamwe hawajakuwa ni kikundi cha Siasa tu.
Walikuwa wakati wote wanaunda madhehebu ya dini, ambayo hayakuanzishwa, katika wakati wa Ukhalifa wa Uthman, lakini lililinganiwa kutokana na maneno na maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika wakati wake mwenyewe.

Wakati ambapo wapinzani wa Shia hujadili kwa msingi wa ushahidi wa kubuni wa maadui, mimi nitanukuu kwa ajili yako Aya kutoka Qur’ani Tukufu na similizi za waandishi wenu wenyewe kuonyesha hali ya ukweli halisi.

Maana Ya Neno Shi’a
Shi’a kama ujuavyo, kilugha ina maana ya “Mfuasi.” Mmoja wa maulamaa wa kisunni, Firuzabadi katika kitabu chake “Qamusu’l-lughat,” anasema: Jina la Shi’a kwa kawaida lina maana ya kila mtu ambaye ni rafiki wa Ali na Ahlul-Bait wake.
Jina hili ni lao peke yao.” Maana hii hii hasa inatolewa na Ibn Athir katika “Nihayatul’l-Lugha.” Kutokana na Sharh za kisunni, neno Shia lina maana ya “wafuasi wa Ali ibn Abu Talib,” na lilikuwa likitumika katika njia hii katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kwa kweli alikuwa ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe ambaye alilitambulisha neno Shi’a kwa maana ya “Mfuasi wa Ali bin Abu Talib.” Na neno hili lilikuwa likitumiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye kuhusu yeye Allah (s.w.t.) Anasema:
 “Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.” (53: 3-4)


Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita wafuasi wa Ali “Shia,” “waliokombolewa” na “waliookolewa.”

Comments