SHEREHE ZA IDDIL F ITRI
Allah (s.w) anasema “Hakika
wabadhirifu ni ndugu zake mashetani; na Shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake”
(Al-Isra : 27). Ama wakati wa kuimaliza Ramadhani, katika pilika pilika za
furaha ya sherehe za Iddi, utajionea mwenyewe namna mwanadamu anavyoghilibiwa
kwa haraka na kuchezewa shere na Shetani. Hayo utayashuhudia katika beach,
sinema na hata katika tamasha za disco na dansi - na Mungu atuepushe.
Ni kweli kwamba, Mtume (s.a.w.w)
alisema, “Mambo mema huyafuta maovu” Lakini papo hapo maovu nayo huyafuta mema.
Sheikh mmoja alipokuwa akisoma darasa
msikitini alisema, “Mwenye kulisema neno hili ‘Laahaula Walaa Quwwata Illaa
Billahil Adhim’ mara moja tu, Mwenyezi Mungu Humpandia mti wa mtende peponi. Na
kila msomapo hupandiwa na hivyo basi kuifanya idadi ya mitende apandiwayo kuwa
sawa na idadi ya mara alizosoma.”
“Si mitende hiyo itaijaza pepo hata
kukosekana nafasi?” Aliuliza mmoja wa waliokuwepo. Sheikh akamjibu “La,
haitajaa maana hata mashoka ya kuikata na kuibwaga chini ni mengi. Kwa mfano:
Mtu aliyepandiwa mti huo baadaye atasengenya, au akadanganya, au akafanya kosa
lolote lile na kila kosa afanyalo huwa mtende mmoja wabwagwa. Jee! mtu huyo
atabakisha kitu?
Na vivyo hivyo sisi lau tutausahau
wajibu wetu wa kumtii na kumnyenyekea Mwumba wetu, bila shaka tutakuwa taabani
hapo kesho tutakapotiwa adabu." Hakuna faida yoyote ile kwa mtu kushinda
mchana kutwa au mwezi mzima akiabudu na kufika usiku au siku ya kufuturu
akaasi, maana kufanya hivyo kutakuwa sawa na aliyepeleka Benki Shs. 100,000/-
na kabla ya kuzifikisha akazitumia zote. Je, mtu huyo ana kitu alichoweka?
Kesho Jumamosi ni siku ya Idd kwa
sisi waislamu. Japokuwa wanafiki wa kiwahhabi wamesherehekea idd siku ya
Ijumaa. Katika sherehe hii tuendelee kufanya ibada. Katika siku ya idd na miezi
mingine yote ijayo, kwa sababu Ramadhani tunayoimaliza Jumamosi ni chuo cha
ucha Mungu na siku ya idd ndio sherehe ya mahafali. Tunapohitimu tunatakiwa
tuwe na maarifa na juhudi zote za kutufanya tuendelee kuwa wacha Mungu.
Eid Mubarak
Comments
Post a Comment