SIFA ZA SURA AL-HAMD
(AL-FATIHAH)
Miongoni mwa Sura za
Qur’ani Tukufu, Sura hii inayo hadhi ya juu, ambayo hunyanyuka kutoka kwenye
sifa zifuatazo:
1. Uzito
wa Sura hii:
Kimsingi, sura hii inayo
tofauti iliyo wazi na sura zingine za Qur’ani Tukufu kutokana na mtazamo wa
uthabiti na uzito, kwa sababu sura zingine zote zinatoka kwenye usemi wa Mungu
ambapo Sura hii inatoka kwenye ulimi wa waja. Na kutoka
kwenye Mtazamo mwingine katika Sura hii, Mungu amewafundisha waja wake namna ya
kusema na kuwasiliana na Yeye”
Utangulizi
wa Sura hii umeanza na kumsifu na kumtukuza Mola Mlezi.
Inaendelea
na imani mwanzoni na baada ya maisha ya hapa duniani (kumtambua Mungu na imani
katika ufufuo), inaisha na mahitaji na masharti ya waja.
Wakati mtu mwenye
hadhari, ambaye moyo wake umezinduka anasoma sura hii huhisi kwamba amewekwa
kwenye mabawa na manyoya ya malaika, kwamba ananyanyuka kwenda mbinguni, na
kwenye uwanja wa kiroho, hatua kwa hatua, anasogea karibu zaidi kwa Mungu
(s.w.t.).
Hili
ni wazo bora sana, kwamba Uislamu, katika kukinzana na mifumo mingi ya
imani za uongo (ambapo husemekana kwamba wapatanishi wameteuliwa kati ya Mungu
na viumbe,) umetangaza kwa wanadamu kwamba bila ya mpatanishi wanatakiwa
kuanzisha uhusiano na Muumbaji wao!
Sura
hii ni mfano, ambamo uhusiano huu wa karibu kati ya Mungu na wanadamu
imeegemezwa (bila ya wapatanishi), kati ya vilivyoumbwa na Muumbaji. Mahali
hapa yeye (mja) humuona Yeye tu, husema Naye tu, husikiliza ujumbe Wake kwa
masikio yake na mwili wake, hivyo kwamba hapana hata Mtume au Mjumbe au mmoja
wapo wa Malaika wa karibu sana anakuwa mpatanishi katika uhusiano huu. Na
inastaajabisha kwamba muunganiko huu na uhusiano wa moja kwa moja wa vilivyoumbwa
kwa Muumbaji ni mwanzo wa Qur’ani Tukufu.
Comments
Post a Comment