SWALA (IBADA) NI NINI?
Sala ni matendo na maneno ambayo hujenga mahusiano kati ya Muumba na kiumbe,
hivyo mja akiikata, basi mawasiliano yake na Mola wake hukatika.
Allah Mtukufu anasema: “Kwa hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu hakuna
aabudiwaye ila Mimi tu, basi niabudu na simamisha Swala kwa kunitaja” (Surat
Twaha: 14).
Kila mtu mwenye akili timamu ni lazima atafute utaratibu sahihi wa
kuwasiliana na Muumba wake na autumie huo kwa kazi hiyo. Kuna wengine wengine
huimba sana na kudai kuwa hiyo ni sala, lakini kwa hakika hizo ni starehe na
wala sio ibada. Kuna watu wengi pia huwaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, hilo
nalo ni kosa kwa sababu wanapoteza nguvu zao bure kwani hivyo wanavyoviabudu
havitowafaa kwa lolote.
Hivyo basi tumtambue Mwenyezi Mungu Muumba mbingu, ardhi na kila
vilivyomo, huyo ndiye anayestahihili kuabudiwa peke yake.
Comments
Post a Comment