SWALI LA KWANZA KWA MAWAHHABI NA MASALAFI

SWALI LA KWANZA KWA MAWAHHABI NA MASALAFI
Hitoria inashuhudia kuwa wakati Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipotangaza utume wake, yeye na ukoo wake (Bani Hashim) waliwekewa vikwazo vikali sana. Waliofanya hivyo ni Maquraish.


Mzee  Abu Talib (as) aliliupeleka ukoo wake katika eneo liitwalo Shib Abi Talib ambapo alijificha hapo kwa miaka mitatu, wakiteseka kwa njaa kali na shida za kila aina. Kiasi kwamba walifikia hatua ya kula ngozi za viatu vyao kwa sababu ya njaa.

Wakati huo Sayyidna Abu Bakar na Umar wakiwa mjini wakiponda raha. Je huu ndio Uislamu wa watu hawa? Kwa nini hawakumsaidia Mtume na ukoo wake katika kipindi hiki kigumu? Kama wangeshindwa kujiunga naye pangoni wangewapelekea walau chakula. Lakini hakuna ushahidi unaoonesha kuwa waliwapelekea chakula wala nguo. Na kama wangekuwa wakiwapelekea wasingepata shida kubwa kiasi hicho kwa sababu wote wawili walikuwa na uwezo wa kutosha.  

Maquraish ikiwa ni pamoja na Abubakar na Umar walikutana na kukubaliana kuwa wasifanya biashara yoyote na Bani Hashim na bani Mutalib na wasioleane na mkataba huo ukaandikwa na kubandikwa ndani ya Alqa’bah, na wakaahidi kuutekeleza kiukamilifu. Bani Hashim na Bani Mutalib wote walikwenda kumzunguka mzee Abu Talib (baba wa Imam Ally) katika bonde lake isipokuwa Abu Lahab aliyejiunga na Maquraish na kushirikiana nao katika vita vyao dhidi ya Mtume na Ukoo wake.

Rejea:
1. Tarekh Tabari ya kiingereza vol. 6 ukurasa wa 81

2. Siratun Nabi cha Shibli Numani vol. 1 ukurasa wa 218 (tafsiri ya kiingereza ya M. Tayyib Bakhsh Budayuni).
Katika kitabu hiki ameonyesha kuwa walikuwa na njaa kali kiasi cha kula majani ya miti iliyokuwa hailiwi kabla ya hapo na migomba.

Haya tuelezeni wale mnaodai kuwa walikuwa marafiki wakubwa wa Mtume walikuwa wapi? Kwa nini hawakumsaidia? Mtu (Abu Talib) mnayemsingizia kuwa ni kafiri ndiye alikuwa akikesha kumlinda Mtume wakati waheshimiwa wakistarehe, je huo ndio Uislamu mnaousifia? 

Comments