TENDO BORA KUFANYWA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI

TENDO BORA KUFANYWA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI
Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s) alimuuliza Mtume (s.a.w.w): “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni tendo gani lililo bora kabisa katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani?” Mtume Mtukufu (s.a.w.w) alijibu: “Ewe Abu’l Hassan, bora ya matendo yote katika mwezi huu Mtukufu ni kujiweka mbali kabisa na yale yaliyoharamishwa na Allah S.W.T

 “Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu. Siku chache tu (kufunga huko). Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au katika safari (akafungua baadhi ya siku), basi (atimize) hesabu katika siku nyingine. Na wale wasioweza, watoe fidia kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa radhi ya nafsi yake, basi ni bora kwake. Na (huku) kufunga ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (haya sasa basi fuateni) Al-Baqarah: 183-184.

Kwa hiyo mwezi mtukufu wa ramadhani umetengwa na Allah (s.w) ikiwa ni uwanja muhimu kwa waislamu kufanya mazoezi ya uchamungu. Inategemewa kuwa tukimaliza mwezi huu tutaendelea na tabia hizo hizo za kichamungu.


Tunamwomba Allah (s.w) atuimarishe katika dini yetu na atufishe tukiwa na waislamu na watufanye kuwa wacha Mungu. 

Comments