TOFAUTI
ILIYOPO BAINA YA AHLU-SUNNA NA SHIA (ITHNA ASHARI).
Kuna tofauti baina ya Sunni na Shia
katika mas-ala mbali mbali ingawa wote wanaunganishwa na kitu kimoja ambacho
ni: Dini Tukufu ya Uislaam. Wote dini yao moja ni Uislaam lakini tofauti ndogo
zipo baina yao katika baadhi ya Mas-ala.
Tofauti kuu iliyopo baina ya Sunni na
Shia ni hii ifuatayo:
Ahlu-sunna ambao hujulikana sana sana kwa walio wengi kama (Masunni) hufuata Makhalifa wanne (4) ambao wa kwanza wao ni Abu Abakar bin Kuhafa,na baada ya hao wanne hufuata Makhalifa wote wa Bani Umaiyya (yaani: Makhalifa wale wanaotokana na kizazi cha Bani Umaiyya, nadhani ndugu msomaji utakuwa unaelewa ni akina nani hao bani umaiyya, historia imewaelezea vizuri bani umaiyya, hivyo hatutaelezea sehemu hii ni nani huyo Umaiyya na ni akina nani hao bani Umaiyya!).
Hivyo Ahlu-sunna wanafuata Makhalifa 4 wa mwanzo wa kwanza wao akiwa Abu bakari na wa Mwisho wao akiwa Imam Ali (a.s), kisha baada ya hao wanafuata Makhalifa wote wa Banu Umaiyya, hata kama atakuwepo miongoni mwao Khalifa ambaye ni dhalimu wao wanaamini ni wajibu kufuatwa dhalimu huyo na udhalimu wake sio sababu ya kutofuatwa, kwa ibara nyingine: Uadilifu wa Khalifa sio sharti la kukubalika kwake, bali anaweza kuwa Khalifa na ni wajibu kufuatwa hata kama atakuwa dhalimu na muovu.

Lakini Shia Ithna Ashari, wao ni
wafuasi wa Maimamu Maasumini Kumi na wawili (12) (a.s) kutoka katika Kizazi cha
Mtukufu Mtume (s.a.w.w),hao ndio viongozi wao.
Hivyo Mashia hawaamini Makhalifa zaidi
ya kumi na wawili (12) wala idadi pungufu ya kumi na mbili, maana hadithi ya
Mtume (s.a.w.w) inasema Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili(12), haisemi
kuwa makhalifa baada yangu ni wanne (4) au zaidi ya 12.
Hivyo
Mashia wanaona kwamba: Kuamini au kufuata Makhalifa wanne Abubakari, Omar, Uthamn
na Ali, ni kinyume na hadithi ya Mtume (s.a.w.w), maana hadithi hiyo haijsema
kuwa Makhalifa ni wanne, bali imesema ni kumi na wawili(12), na akijitokeza mtu
akasema: Sunni tunaamini Makhalifa wa kwanza wanne, kisha tunaamini ukhalifa wa
makhalifa wa Banu Umaiyya, basi Shia Ithna ashari hujibu kunako hilo kuwa: Makhalifa
wa Banu Umaiyya idadi yao ilikuwa zaidi ya 12, wanafika 100 na zaidi, kwa hiyo,
hiyo nayo itakuwa ni kwenda kinyume na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) kuwa
Makhalifa baada yake ni kumi na wawili (12), kwa maana kwamba; Makhalifa
hawatakiwi kupungua wala kuongezeka katika idadi hiyo iliyotajwa na Mtume
(s.a.w.w) katika hadithi sahihi iliyopokelewa na madhehebu zote za kiislaam.
Hii ndio tofauti kuu inayopatikana
baina ya Shia Ithna Ashari na Ahlu-sunna.
Kunako
tofauti hii unaweza kurejea kitabu kiitwacho:
Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya: Juzuu ya 2; ukurasa wa 11-12.
Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya: Juzuu ya 2; ukurasa wa 11-12.
Comments
Post a Comment