TUKIO LA KARATASI KATIKA ZAMA ZA MTUME (S.A.W.W)

TUKIO LA KARATASI KATIKA ZAMA ZA MTUME (S.A.W.W)
Waandishi wa tarikh na Hadithi wamelieleza tukio la Karatasi kama hivi: "Mtume (s.a.w.) alipokuwa mgonjwa mahututi, watu wengi walikusanyika ndani ya nyumba ya Mtume akiwamo Umar Ibn Khattab (r.a).
Mtume (s.a.w.) aliwaambia kuwa: "Nileteeni Karatasi niwaandikieni maandiko hamtapotea baada yake." Umar akasema: Mtume anaweweseka! Mtume akawaambia: "Niondokeeni" wakaondoka.
Katika kauli nyingine inasema: Umar alimwambia Mtume baada ya kuagiza karatasi: "Mtume yamemzidi maradhi inakutosheni Quran mliyo nayo". Kauli ya kwanza na ya pili utazipata katika: Sahih Bukhar Kitabul Ilmi, Sahih Bukhar Kitabul Tibb, Sahih Bukhar Kitabun Nabi ila Kisra, Sahih Bukhar Babu Karahiyatul Khilaf, Sahih Bukhar Babu Jawaizil wafdi, Sahih Muslim Babu Tarikil Wasia, Tarikhut Tabari Juzu.2 Uk., 436 Sharhush Shifaa Juxu.2 Uk. 353


Mwenyezi Mungu anasema: "Wala (Mtume) hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake) hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa." (53:3-4).
Amesema Abdallah bin Amri: "Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kwa Mtume Muhammad (s.a.w.) ili nikihifadhi, Makuraishi wakanikataza wakanambia: Wewe unaandika kila kitu unachokisikia kwa Mtume!? Na Mtume ni binadamu, anazungumza (wakati mwingine) katika hali ya ghadhabu. Basi nikajizuia kuandika, nikamjulisha hayo Mtume (s.a.w.). Akasema Mtume, "Andika, na muapa yule ambaye nafsi yangu imo katika milki yake, mimi sisemi isipokuwa haki tupu". Taz: Tafsir Ibni Kathir J.4 Uk. 264, Tafsir Maraghi J.27 Uk. 45
Somo hili linatufundisha kuwa: Wakati wote Mtume (s.a.w.) anaposema, huwa ni Wahyi. Sawa sawa awe katika furaha kubwa au katika ghadhabu, na awe katika maradhi au afya.
Sasa: kwa nini Umar alizuia usiandikwe Wahyi na nini hukumu ya mtu kama huyu? Sikiliza, Mwenyezi Mungu anasema: "Atakaempinga Mtume baada ya kudhihirikiwa muongozo, na kufuata njia isiyokuwa ya waumini, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe, na tutamwingiza katika moto wa Jahannamu." 4:115.
Ninapenda kumpa pole Umar bin khatab na wafuasi wake wote duniani ambao wanatumia muda wao mwingi kumtetea na kupambana na kila atakaye sema ukweli kumhusu Umar.
Lakini ni dhahiri kuwa matendo ya kiongozi huyu wa kiwahabi yalikuwa ya kiwahhabi kweli kweli, ujeuri juu ya ujeuri. Hakuweza kuiona Heshima ya Mtume (s.a.w.w) na kuipa hadhi inayostahili. Inawezekana ndio maana wafuasi wake ni watu wakorofi na wakali kwa mambo madogo madogo kiasi kwamba ni vigumu kuwafahamu kuwa ni waislamu wa kweli. Bila shaka ujeuri wao unatoka kwa kiongozi wao huyu aliyekuwa hana adabu kwa Mtume. Je mtu aliyekuwa na adabu kwa Mtume atakuwa na adabu kwa nani tena?

Comments