UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA
Udhuu ni tendo la kunawa (kutawadha) kisheria kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Swala. Swala ni nguzo kubwa ya dini haikamiliki mpaka mtu awe na Udhuu:
Allah (s.w) anasema, "Enyi! Ambao mmeamini mnapokusudia kuswali osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye viwiko, na pakeni sehemu za vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili…"(al-Maidah; 5: 6).

Aya hii ndio aya inayotufundisha sisi namna ya kutekeleza ibada hii muhimu ya kuchukua udhu.

Kwa bahati mbaya kuna tofauti ya jinsi ya kutawadha kati ya Shi'a na Sunni kiasi kwamba kila mmoja anamshangaa mwenzake, hususani mwiongoni mwa wafuasi. Wengi wa wanachoni wa Kisunni wamejuzisha kukosha miguu, ambapo wanachuoni wa Kishi'a wamejuzisha kupaka miguu.

Imekuwa in kawaida ya watu kukubali kila jambo linalofanywa na watu katika jamii wanayo ishi bila ya kuhoji ubaya au uzuri wa jambo hilo. Lakini hii yote ni kwa sababu ya kutojuana
na kutotaka kujuana.


Mimi nitafanya uchambuzi wa kina kuhusu suala hili. Tafadhali, ninaomba tufuatane katika kazi hii adhimu bila jazba wala taasubu.

Comments