UHARAMISHO
WA KUSEMA UWONGO
Allah (sw) anatuambia katika Qur'an Tukufu Surah
An-Nahl 16, Ayah ya 105:
'Wanaozua uwongo hawana imani'
Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: "Mtu
mwovu kabisa ni yule ambaye ni msema uwongo."
Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: "Allah (sw)
humlaani mwongo hata kama atasema ukweli"
Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) (Imam wa kwanza wa
Shia). amesema: "Ugonjwa wa kusema uwongo ndio ugonjwa mbaya kabisa."
Amesema al-Imam Musa ibn Ja'afar (a.s) (imam wa saba
wa Shia). : "Mtu mwenye busara kamwe hawezi kusema uwongo hata kwa
matamanio yake mwenyewe."
Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: "Itakuwa
vyema kwa Waislamu iwapo hawatafanya urafiki na udugu pamoja na Mwongo."
Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir (a.s) (imam wa tano
wa Shia), katika Al-Kafi, j.2: "Uwongo unateketeza misingi ya Imani."
Mashia kama waislamu tunaamini kuwa Mwanadamu ameumbwa
kwa maumbile ya ukweli na uaminifu. Iwapo yeye ataweza kudumisha maumbile hayo
bila ya kushawishiwa na vitu vya nje na mambo yanayomvutia, basi daima atasonga
mbele katika wema na utakatifu, na kuepukana na maovu na machafu.
Mwanadamu kimaumbile ni mkweli, mwaminifu, mtukuzwa na
mwadilifu. Lakini kuna mambo kama elimu, mazingira n.k. yanaweza kuathiri sifa
hizi na kuzibadilisha kwa maovu.
Uwongo ni
kinyume na maumbile ya kibinadamu na hivyo humvuta mbali na uaminifu na kuna
uwezekano kuwa mwongo na mwovu, na inaweza kuwa ni kama ugonjwa ulioambukizwa
na kuenea kutoka kwa baba hadi vizazi vyake, kutoka mwalimu kwa wanafunzi wake,
kutoka mnunuzi kwa muuzaji na kuendelea, na hivyo kugeuza maumbile kutoka vile
ilivyokuwa imeumbwa.
Comments
Post a Comment