USHAHIDI WA MTUME KUTANGAZA KUWA UISLAMU UTAONGOZWA NA
MAIMAMU 12.
Jabir bin Samura alisimulia kuwa alimsikia Mtume (s.a.w.w)
akisema kutakuwa na maimamu kumi na mbili na wote watakuwa Makuraish Bani
Hashim.
Soma sahihi Bukhari ya kiingereza, kitabu Ahkam,
hadith namba 9329,
Sahihi Muslimu ya kiarabu, juzuu ya 4 ukurasa 165
kitabu Ahkam.
Mtume (s.a.w.w) alisema Uislamu utaendelea kuwepo
mpaka siku ya kiama na utaongozwa na maimamu 12, wote Maqraish.
Soma: sahihi Muslim ya kiingereza, juzuu ya tatu,
ukurasa 1010, hadith namba 4483.
Sahihi Muslimu ya kiarabu, kitabu Imaara
kilichochapishwa Saudi Arabia mwaka 1980, juzu ya 3 ukurasa 1453, hadith namba
10.
Al-dhahabi katika kitabu chake Tadhikirat Huffaz juzu
4 ukurasa 298 na ibn Hajjar Al-Asqaran katika Al-Duar al-Kaminah juzu 1,
ukurasa wa 67: wanasema kuwa Abdillah ibn Abasi (R.A) alisema kuwa Mtume (s.a.w.w)
alisema mimi ni kiongozi wa Manabii na Ally bin Abutalib ni kiongozi wa
maimamu, na baada yangu maimamu watakuwa 12 wa mwanzo wao atakuwa Imamu Ally
ibn Abitalib na wa mwisho wao atakuwa Mahdi.
Huu ni ushahidi tosha kuwa Mtume (s.a.w.w)
aliwatangaza Maimamu 12. Kama utahitajika ushahidi zaidi ya huo upo tutauleta
insha-Allah. Maimamu hawa ndio wanaofuata na Mashia ithnaashara peke yao.
Comments
Post a Comment