UTUME (MZIZI WA DINI)
Kwa ujumla dini ya Mtume Muhammad
Mustafa (s.a.w), ni dini ile ile waliyokuja nayo Mitume waliopita kabla ya
yeye, kuanzia Nabii Nuhu (a.s) mpaka kufikia Nabii wa mwisho Mtume Muhammad
(s.a.w), basi Mitume wote ni Mitume wa Mwenyeezi Mungu mmoja, Mola ambaye ndiye
mwenye ufalme wa nyumati zote za Mitume hao, vile vile Mitume hao wamekuja na
dini moja pamoja na lengo moja, nalo ni kuwaalika wanaadamu wamuabudu Mola
mmoja wa haki.
Tutaweza kuyathibitisha
hayo kama tutazingatia Aya ya 42-92 ya Suratul-Anbiyaa, aya za sura
hiyo zimeelezea kwa uwazi kabisa kuwa Mitume hao walikuwa na lengo moja la
kuwaongoza watu katika njia moja, na waumini wote (Waislamu) ni umati mmoja.
Hivyo basi dini zote ambazo ziko nje
ya Uislamu zimepatikana kutokana na kazi ya shetani. Ndivyo hivyo hivyo kwa
upande wa madhehebu. Kama mungu ni mmoja na Mtume wa mwisho ni mmoja haiingii
akilini kuwepo na madhehebu mengi. Inambidi kila mwanadamu afanye uchunguzi wa
kina kuhusu usahihi wa madhehebu yake. Kwa sababu nyingi ya madhehebu ni
ubatili na matunda ya shetani katika kuwaondoa wanadamu toka kwenye njia
iliyonyooka.
Comments
Post a Comment