UTUMWA MAMBO LEO:

UTUMWA MAMBO LEO:
Dunia imegubikwa na Utumwa mamboleo unaoendeshwa na nchi za Magharibi na vibaraka wao. Uendelezaji wa wazi wa aina za utumwa unaweza kufanikiwa kwa njia ya kusaidia Mipango kama vile “Millenium African Recovery Plan.” Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za uzalishaji unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi National Cartels) tayari upo.

Mfumo huu hupenya kwenye kila tabaka la uchumi wa dunia, iwe ni bidhaa zinazo zalishwa, kama sukari, silaha za kivita, madawa ya tiba au biashara ya dhahabu na madini ya platinamu.

Utumwa wa kiuchumi kupitia udhibiti mtiririko wa mitaji ulimwenguni uko imara mikononi mwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Uharibifu kwa Afrika ulitokea kwa njia ya utawala wa mabavu wa kikoloni wa moja kwa moja, uliofanywa na Uingereza, Udachi, Ufaransa, Ureno na Ubeligiji. Hii ilifuatiwa na udhibiti wa nje ya Afrika, kwa kuanzisha serikali kidhalimu ili kuendelea kudhibiti kwa njia za hila zaidi. Kwa kufichuliwa vibaraka hawa kwa ajili ya ulimwengu kuwaona, ikawa vigumu zaidi kuendelea kwa uwazi kusaidia vitendo vyao viovu dhidi ya jamaa zao. Vurugu zilidhibitiwa ili kuhakikisha kuendelea uingiaji kwenye akiba kubwa za madini.
Njia changamano ilikuwepo kazini kwa zaidi ya miaka 30, ambayo ni kulitumbukiza bara hili (la Afrika) kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na maana yoyote. Ahadi za “kusamehe madeni” zinatolewa kwa lengo la kuendeleza utumwa kwa Waafrika. Huu “Utumwa Mpya” unaweza kuonekana tofauti kwa nje na ule wa “West
African Slave Trade” (Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi), lakini misingi yake inafanana.

Kwa kuanzishwa kwa mfumo wa makao makuu ya fedha (Benki ya Dunia na shirika la Fedha la Kimaraifa), Polisi wa Dunia (North Atlantic Treaty Organization), imewarahisishia wakoloni kazi ya kuwa na mamlaka ya kuitawala Afrika.

Mfano wa wazi unaoonyeshwa na nguvu hizi za wakoloni na washirika wake, ni kuunda taifa la Israeli katikati ya Rasi ya Arabia. Kwa hiyo ni muhimu sisi kuchambua na kuonyesha ulinganifu huu baina ya Uzayuni
(Zionism) na washirika wake na ukubwa na vipimo vya utumwa unaoendelezwa na nguvu za wanyonyaji.

Tutaendelea kutoa mada kuhusu kadhia hii ya ukoloni ili watu wajue namna wanavyotumiwa katika kuwanyonya wao wenyewe na ndugu zao. Ni vigumu kuelewa mikakati ya maharamia hawa endepo kama usifanya uchunguzi wa kina.

Utakuta ndugu zetu mawahhabi na masalafi wametumika sana kuwasaidia wakoloni katika juhudi zao za kuitawala dunia. Utakuta kila anayeipinga Israel na Ulaya anapigwa vita na Mawahhabi wa Daesh, ISIS, Jabhat Annusra, Alqaidah na Boko Haramu. Kama kweli wao wanapambana na utumwa na umagharibi kama wanavyosema kwa midomo basi wangeenda kupambana nao nchini kwao badala ya kuwauwa waislamu katika nchi zao wenyewe au kusafirisha magaidi kutoka ulaya na kuwapeleka mashariki ya kati kuwalipua watu.

Comments