WAISLAMU WAAGIZWA KUISHI VYEMA NA WATU WA DINI NYINGINE

WAISLAMU WAAGIZWA KUISHI VYEMA NA WATU WA DINI NYINGINE
Ingawaje sisi Waislamu tuna itakidi ya kuwa dini ya Kiislamu ndiyo dini pekee iliyo rasmi katika zama hizi tulizonazo, lakini vile vile tunaamini ya kuwa ni lazima tuishi kwa salama na amani na wafuasi wa dini nyengine, inawezekana wafuasi hao wakawa wanaishi katika nchi za Kiislamu, au pia wakawa hawaishi katika nchi za Kiislamu, isipokuwa kwa wale wanaopinga na kupiga vita dini ya Kiislamu.

Allah (s.w) anasema katika Qur,an kuwa Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu (Surat Mumtahinah Aya ya 8).

Sisi tunaamini ya kuwa; ikiwa dini ya Kiislamu itaarifishwa kimantiki, basi kutakuwa na uwezekano wa kuibainisha kwa uwazi dini hiyo kwa watu wote duniani, na kwa sababu dini ya Kiislamu ina dalili zenye nguvu na zinazokubalika kiakili na kimantiki basi kuna uwezekano wa kuwaongoa watu wengi duniani, katika dunia ya leo watu wengi wana kiu ya kusikia ujumbe wa dini ya Kiislamu.


Hivyo basi Uislamu ni dhahabu inayotafutwa na kila mtu, kinachofanywa na Mawahhabi kuwaua watu kwa madai kuwa sio waislamu au kwamba ni watu wa bid’a ni ukafiri waliokubuhu na usiokubalika ndani ya Uislamu. 

Comments