ATHARI ZA SWALA NA SIRI ZAKE:

ATHARI ZA SWALA NA SIRI ZAKE:
i. swala huleta utulivu wa nafsi
“Kwa hakika binadamu ameumbwa hali ya kuwa mwenye pupa.
Inapomgusa shari huwa mwenye fazaa. Na inapomgusa kheri huwa
Anaizuilia, isipokuwa wanaoswali.” (Sura Al-Maarij: 19 - 22.)

ii. Swala ni kinga ya muumini
“Na ombeni msaada kwa subira na Swala na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.”( Sura Al-Baqarah: 45)

iii. Swala ni njia ya mafanikio na ukamilifu
“Na simamisha Swala katika sehemu mbili za mchana na nyakati za usiku, hakika mema huyaondoa maovu, huo ndio ukumbusho kwa wenye kukumbuka.” (Sura Hud: 114)
“…Bila shaka Swala huzuia mambo machafu na maovu…”( Sura Al-Ankabut: 45)

iv. Swala humfundisha binadamu mipango na nidhamu katika maisha

“…Hakika Swala kwa wenye kuamini ni faradhi iliyo na wakati maalumu.” (Sura An-Nisai: 103)

Comments