BALEGHE
Mwanzoni mwa kipindi cha
ujana hutokea mabadiliko makubwa na ya kina ambapo nguvu za kimwili na kiroho hufunguka. Si
hivyo tu, bali katika kipindi hiki ndani ya akili ya mwanadamu huchomoza
matarajio na fikra mpya na kumwonesha kuwa anayo hadhi inayowavutia wengine
kushirikiana naye.
Bila shaka kuanzia hapo mtu
huyu hukataa kuwa (mwenye) kufuata tu, ambapo sasa hutafuta uhuru katika mambo
yake binafsi na katika maamuzi yake anayoyachukua. Hali hiyo humaanisha kuwa
amefikia kipindi cha Baleghe na kuwa anataka kuchagua njia moja baina ya njia
nyingi mbali mbali.
Na njia hii ni ile itakayo
mfikisha kwenye wema wake binafsi, kama ambavyo ni wajibu wake binafsi
kuichagua njia hiyo, kwani katika bahari hii yenye wingi wa fikra zinazo
gongana huenda akajikuta anamhitajia (mwanachuoni) atakayemsaidia kumuongoza na
kumvusha Salama na kumfikisha ufukweni kwa amani.
Basi ndani ya kipindi hiki,
huruma ya Mwenyeezi Mungu humfunika na rehema humteremkia kwa msaada wa ujumbe,
hapo ni bora kijana akisome sana kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwe muongozo
wake.
Kwa hali hii basi, mara
atajikuta anahisi furaha na kuingia katika mazingira mazuri hali ya kuwa uso
wake ni wenye nuru na huku ulimi wake ukimhimidi na kumshukuru (Mola) juu ya
yale aliyoelezwa na kule kufikia kipindi cha kuwajibika kisharia.
Hakika Baleghe ni kitabu cha
habari na matendo ambacho ni lazima kukihifadhi ili nuru yake idumu na usafi wa
kurasa zake uendelee mpaka mwisho wa uhai. Hakika siku ya kubaleghe ndiyo siku
ambayo Malaika wana haki ya kukaa kushotoni na kuliani: “Hatamki neno ila
karibu yake yupo mwangalizi tayari.” Na hali ya kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu
inamjumuisha inasema: “Enyi Mlioamini…..”
Hapa ni lazima kijana
aongeze juhudi katika dini kwa sababu hukumu za Allah zinambana na akitenda
jema hulipwa na pia akitenda uovu atalipwa kwa hilo.
Comments
Post a Comment