FUATA HAKI NA USITEGEMEE KUWA HAKI ITAKUFUATA WEWE
Assalaam alaykum:
Mambo yanayoweza kuamsha misimamo ya watu na kuleta msukumo mpya katika kumwandaa binadamu ili apige hatua mbele, ni kujua habari za watukufu wao waliotangulia. Kwa sababu kujua habari za watangulizi wetu ni mizani ya kutupimia sisi tunaokuja baada yao. Nimeweka mada nyingi, wanaojua kuwa ni kweli si kidogo, lakini wengi wanaogopa kuyasema au wametiliwa itikadi potovu kuwa hayafai kusemwa. Bila shaka, watu wa aina hiyo wanaamini kuwa mimi ninafanya makosa kueleza Historia na Mtukio muhimu yaliyotokea katika kipindi cha Mtume (s.a.w.w) na baada yake na kwamba itakuwa ni dhambi kubwa kwao kuyasema.

Sisi nasi tunaamini kuwa Haki ni lazima isemwe, sawa
sawa itawaridhi watu au haitawaridhi. Allah (s.w) anasema, "NA LAU HAKI
INGEFUATA MAPENZI YAO BASI MBINGU NA NCHI ZINGEHARIBIKA" (23:71).
Ninawashukuru
wote wanaozisoma mada zangu na kuzijadili kwa wema, na wakanipa maoni yao yenye
thamani kubwa. Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema duniani na akhera.
Mwalimu Rajabu Shaban Kabavako
Comments
Post a Comment