ITIKADI YETU WAISLAMU KUHUSU TAUHIID.

ITIKADI YA WAISLAMU KUHUSU TAUHIID.
Umma wa Kiislamu tangu mwanzoni umeshikamana juu ya Tauhudi katika nyanja zake mbali mbali, ukaafikiana juu ya kuipwekesha dhati ya Mwenyezi Mungu na kwamba, yeye ni mmoja hana mshirika wake na ni mpweke hana mfano.
Kama ambavyo umeafikiana ya kwamba, yeye ni Muumba na hapana muumba asiyekuwa yeye.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu"
Qur'an, 35:3
Na Amesema tena:
"Waambie, Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu"
Qur'an, 13:16.
Vile vile umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola wala mwenye kusimamiya (mambo yao) asiyekuwa yeye.
Amesema Mwenyezi Mungu:
Yeye ndiye anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idhini yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu?
Pia wamekubaliana kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hukuna wa kuabudiwa asiyekuwa Yeye.
Mwenyezi Mungu Amesema:
"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu".
Qur 'an, 3:64
Bali hizi ndizo nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria zote za mbinguni, na yote haya yanaonekana kuwa ni miongoni mwa mambo ya kipekee kwa baadhi ya wafuasi wa sheria zilizopita. Basi mtazamo ulio kinyume na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotosha vinavyotokana na wanachuoni, Watawa na Makasisi (wao).

 Amma Mawahhabi, Masalafi na Answar Sunnah wana msimamo tofauti na huu. Katika juhudi zao na upotevu wao wamepotoka katika kumtambua Muumba na kumsifia kwa sifa asizokuwa nazo na pia kumpunguzia sifa zake. Itakujia mada mahsusi katika kadhia hii ya Mawahhabi.

Comments