KUMWABUDU MUNGU ASIYEONEKANA
Siku moja Imam Jaafar Sadiq (a.s)
aliulizwa na Kafir kuwa, Vipi viumbe wanaweza kumwabudu Mwenyeezi Mungu ambaye
hawamwoni?
IMAMU akajibu, Nyoyo ziaminizo humwona Mwenyeezi Mungu kwa kufahamu Imani. Wenye hekima hujua kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya hekima zao. Wale wenye maarifa, humwona Yeye kwa sababu ya nidhamu inayolingana ya maumbile na sheria yake. Vile vile, Mwenyeezi Mungu hujulikana kwa sababu ya Mitume, Manabii, Vitabu Vitakatifu na dalili zao. Wanavyuoni wanapotafakari juu ya Utukufu wake, wanajiona kwamba hawawezi kumwona (kuwa ni mwenye umbo).
Kafir akauliza tena: Je, Mwenyeezi Mungu hana uwezo wa kujionyesha binafsi kwa viumbe vyake, ili kwamba kwa kuonekana Kwake, waweze kumfahamu na kumwabudu kwa imani?
IMAMU: Hakuna jibu kwa kitu kisichoyumkinika. Haiyumkiniki, kwa sababu
tendo la kuangalia kitu au kinachoangaliwa huwa wakati miali yake inapofika juu
ya macho (retina) yetu na kufanya taswira yake. Kwa kufanyika taswira ni lazima
kwamba kinachoangaliwa kiwe ni kitu (chenye umbo), ili kwamba kila kijisehemu
chake kidogo kiwe kinatoa mwali wa kufanya taswira. Hivyo, vitu viwili ni
lazima. Kwanza, kinachoangaliwa kiwe ni kitu, Pili, miali ya mwanga ifike
machoni mwetu. Mwenyeezi Mungu ni Mwangaza (Nuru) wa mbingu na ardhi. Mtu
yeyote hawezi kuliangalia jua wakati wa adhuhuri katika Kiangazi, ingawa huwa
ni mwangaza mdogo. Macho ya nani yanathubutu kuangalia mwanga wa Mwangaza
(yaani Mwenyezi Mungu) Ambaye hana kifani? Hivyo, haiwezekani kumuona Yeye.
Isitoshe, kitu kitazamwacho lazima kiwe na "uzito" (dense) kwa ajili
ya kuona na kugusa. Chukua mfano wa hewa. Uzito wake ni mdogo. Ingawa haionekani,
lakini inahisika. Mwenyeezi Mungu hana uzito.IMAMU akajibu, Nyoyo ziaminizo humwona Mwenyeezi Mungu kwa kufahamu Imani. Wenye hekima hujua kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya hekima zao. Wale wenye maarifa, humwona Yeye kwa sababu ya nidhamu inayolingana ya maumbile na sheria yake. Vile vile, Mwenyeezi Mungu hujulikana kwa sababu ya Mitume, Manabii, Vitabu Vitakatifu na dalili zao. Wanavyuoni wanapotafakari juu ya Utukufu wake, wanajiona kwamba hawawezi kumwona (kuwa ni mwenye umbo).
Kafir akauliza tena: Je, Mwenyeezi Mungu hana uwezo wa kujionyesha binafsi kwa viumbe vyake, ili kwamba kwa kuonekana Kwake, waweze kumfahamu na kumwabudu kwa imani?
Comments
Post a Comment