MAONI YA MAWAHHABI NA MASALAFI
KUHUSU UKHALIFA
Maoni yao juu ya Ukhalifa yanaeleweka, nayo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alificha na hakumbainisha yeyote kushika Ukhalifa, lakini watu wenye hekima miongoni mwa Masahaba walikusanyika ndani ya Klabu ya bani Saidah na wakamtawalisha Abubakr ashike mahala pa Mtume (s.a.w.), na hiyo ni kwa sababu Mtume (s.a.w.) alimuachia kusalisha wakati wa maradhi yake, basi wakasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimridhia Abubakar kwa ajili ya jambo la dini yetu basi ni kwa nini sisi tusimridhie kwa mambo ya dunia yetu?
Maoni yao juu ya Ukhalifa yanaeleweka, nayo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alificha na hakumbainisha yeyote kushika Ukhalifa, lakini watu wenye hekima miongoni mwa Masahaba walikusanyika ndani ya Klabu ya bani Saidah na wakamtawalisha Abubakr ashike mahala pa Mtume (s.a.w.), na hiyo ni kwa sababu Mtume (s.a.w.) alimuachia kusalisha wakati wa maradhi yake, basi wakasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimridhia Abubakar kwa ajili ya jambo la dini yetu basi ni kwa nini sisi tusimridhie kwa mambo ya dunia yetu?
Hivyo basi kauli ya Mawahhabina
Masalafi kwa ufupi imefungamana na vifungu vifuatavyo:
1). Mtume (s.a.w.) hakumbainisha
yeyote.
2). Ukhalifa hauwezi
kusihi isipokuwa kwa njia ya mashauriano.
3). Kumtawalisha Abubakr ni
jambo lililotendeka kupitia Masahaba wakubwa.
Bila shaka haya ndiyo yalikuwa
maoni yangu wakati nilipokuwa nikifuata Madhehebu ya Shafii, na nikiyatetea kwa
nguvu zote nilizopewa na nikiyatolea dalili ya aya zinazohusu kushauriana, na
nilikuwa nikijaribu kwa uwezo wangu kueleza kuwa dini ya Kiislamu ni dini yenye
demokrasia katika maamuzi na kwamba yenyewe ndiyo iliyoanza kuweka msingi huu
wa kibinaadamu, msingi ambao mataifa yaliyoendelea yanajivunia.
Zaidi ya hapo nilikuwa nikisema,
"Ikiwa mataifa ya Magharibi hayakupata kuutambua utaratibu huu wa jamhuri
mpaka katika karne ya kumi na tisa, basi bila shaka Uislamu umeyatangulia
mataifa hayo na kuufahamu utaratibu huo tangu karne ya sita.
Lakini baada ya kukutana kwangu
na wanachuoni wa Kishia na kusoma vitabu vyao na kuzichunguza hoja zao zenye
kukinaisha, hoja ambazo zimo ndani ya vitabu vyetu nilibadili maoni yangu ya
mwanzo pale nilipopambanukiwa na hoja zilizo wazi, kwani haiwezekani kwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu kuuacha umma bila ya Imam (kiongozi) kwani yeye Mwenyezi
Mungu ndiye asemaye: "Bila shaka wewe ni muonyaji, na kila kaumu inaye
muongozaji".
Kama ambavyo haistahiki kabisa
kwa mujibu wa huruma yake Mtume kuuacha umma wake bila mchungaji na hasa
tutakapofahamu ya kwamba Mtume alikuwa akichelea utengano[23] wa
umma wake na kurudi kinyume nyume[24] na
kushindania dunia[25] kisa
cha kuuana wao kwa wao[26] na
kufuata nyendo za Mayahudi na Wakristo[27]
Na Iwapo Ummul-Muuminina Aisha
binti Abubakr alimtumia ujumbe Umar bin Al-Khattab wakati alipopigwa dharuba ya
upanga (iliyopelekea kifo chake) akamwambia:
"Mtawalishe mtu juu ya umma wa Muhammad (kabla
hujafa) na usiwaache watu hivi hivi tu, hakika mimi nachelea fitina juu
yao."
Taz: Al-Imamah wa Siyasah.
Na iwapo Abdallah bin Umar naye
anaingia ndani kwa baba yake alipokuwa kapigwa dhoruba hiyo ya upanga na
kumwambia: "Hakika watu wanadai kwamba wewe humtawalishi mtu (baada yako)
basi waonaje lau ungekuwa na mchungaji wa ngamia au mchungaji wa mbuzi kisha
akaja kwako na akaiacha mifugo hiyo bila shaka itapotea, basi usimamizi wa watu
ni jambo muhimu zaidi."
Taz: Sahih Muslim Juz. 6 uk. 5,
Baabul-Istikhlafi wa Tarkih.
Na kama Abubakr mwenyewe naye
ndiye yule Waislamu walimtawalisha kwa mashauriano yeye ndiye anayebomoa msingi
huo na haraka anamtawalisha Umar baada yake ili kwa tendo hilo akate mizizi ya
utengano wa hitilafu na fitna. jambo hili la Abubakr kumtawalisha Umar baada
yake, Imam Ali (a.s.) alilitambua mapema wakati ule Umar alipomlazimisha Imam
Ali ampe Baia Abubakar, basi Imam Ali alisema kumwambia Umar:
"Niandae nafasi ili wewe
uwe na hisa, na leo hii nimuimarishe ili kesho akurudishiye"!
Taz: Al-Imamah Was-Siyasah cha
ibn Qutaibah Juz.l uk.18.
Basi mimi nasema, "Ikiwa
Abubakr hayaamini mashauriano, ni vipi sisi tutaamini kwamba Mtume wa Mwenyezi
Mungu (s.a.w.) aliliacha jambo hili bila kumuweka mtu, na je tuseme Mtume
alikuwa hakijui kile walichokuwa wakikijua kina Abubakr, bibi Aisha na Abdallah
bin Umar? Na ni kitu ambacho watu wote wanakitambua moja kwa moja nacho ni
kutokea hitilafu ya maoni na kila mmoja kutamani namna yake iwapo suala la
kuamua lingeachwa mikononi mwao na hasa pale jambo lenyewe litakapohusu uongozi
na kukalia madaraka ya Ukhalifa".
Rejea zingine:
[24]-
Sahihi Bukhar Juz. 7 uk. 209 Babul-Haud na Juz. 5 uk. 192.
[25] Sahihi
Bukhari Juz. 4 uk. 63.
[26]-Sahih
Bukhar Juz. 7 uk. 112.
[27]-Sahih
Bukhar Juz. 4 uk. 144 na Juz. 8 uk. 151
Comments
Post a Comment