MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU
Mwislamu anatakiwa kuwa sifa za kufanya matendo yafuatayo: Kuwa na
tabia nzuri, Kuwa na elimu, Ushujaa, Unyenyekevu, Huruma na Upole, Kukaa vyema
na watu, Ukarimu, Utawa na Kuwasaidia wanyonge.
Matendo mengine ya mwislamu ni Kutoa Salamu kwa kutangaza (kwa
sauti), Kusubiri, Kukarimu, Kusameheana, Kukidhi haja za watu, Kufanya usawa
kwa kila kitu, Kumcha Mwenyezi Mungu, Usafi, Kuwa na haya, Kuoa, Kuwa na
ukunjufu, Kuwaheshimu watu, Kumshukuru Mungu.
Ni haramu kwa mwislamu kuwa
na matendo yafuatayo:
Kuwaasi na kuwahalifu wazazi, Kuzini, Kufira, Kusagana wanawake,
Kunywa ulevi, Kucheza kamari, Kula mizoga na nguruwe na vinginevyo vilivyo
haramishwa, Kula mali za watu na Kula mlungula (rushwa).
Matendo mengine ya haramu kwa mwislamu ni Kupoteza haki,
Kuiba, Ukuwadi na Kusaidia katika mambo ya ngono hata kwa mke wake, Kusema
uwongo, Kuteta na kufitinisha, Kula Riba, Kuua, Hiyana na Dhulma.
Mwislamu ni haramu Kutumia mali kwa fujo; Kudharau watu,
Kuwaudhi watu, Kutoa siri, Kuficha bidhaa {chakula} ya mahitajio kwa kutaka
kuuza kwa thamani kubwa, Kuwatazama wasio halali na wanawe, Kuhudhuria
mangomani na sinema ya haramu, Kuimba na kusikiliza muziki.
Pia ni haramu kwa muislamu Kujitoa shahawa kwa mkono,
Kuvunja ahadi, Kuvaa pete ya dhahabu na kujipamba wanaume kwa dhahabu, Kuhadaa,
Kughushi, Kupekuwa {upelelezi} mambo ya watu, Kutukana na kushutumu, Kwenda
utupu wanawake kama hali ya sasa, Kumsaidia mdhalimu, Kuhukumu kinyume cha
sheria ya Ki-Islamu.
Tabia
mbaya: Ubahili, Husda. Uwoga,
Kukosahima, Ukaidi na Inadi, Kulipiza kisasi, Kulalamika unapopata msiba, Kutafahari.
Kupenda uongozi na heshima na mali, Pupa, Haraka, Uvivu, Kusema ovyo ovyo,
Kusema upuuzi, Kujidharau. Kiburi, Mghafla. Ufidhuli na Ujuvi, Kuwa na wasiwasi mwingi,
Uchafu, Kukosa huruma, Ulaghai na Ujanja, Kusimbulia.
Nakuombeni
tushikamane na tabia njema na kisha tuepukane na tabia mbaya na tabia za
haramu.
Comments
Post a Comment