MAWAHABI
NA MAUWAJI YA IMAM HUSEN (A.S)
Hebu na tufikirie ni
madhahebu ipi yenye kumtukuza yule mtu Mtukufu ambaye yu Shahidi wa
Karbala na inayozifuata nyayo zake, na ni ipi isiofanya hivyo. Bila ya kusema
mengi, ni madhehebu ya Shia yenye kumwamini Imamu Husayn (a.s.) kuwa yu mtu
aliyeteuliwa na aliyewekwa na Allah (s.w.t.) na yu mrithi wa haki wa nafasi ya
Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Shia wanaamini kwamba kila neno na kitendo cha Imamu
(a.s.) ni katika kumtii Allah, vita yake na amani yake ni kioo cha amali chenye
kufaa, na msimamo wake ndio mapenzi ya Allah.
Kwa Shia, Imamu ni
sehemu ya Nuru (Nuur) ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Nyama na damu ya
Imamu ni nyama na damu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kujitoa kwa ajili ya Imamu ni
jukumu kuu. Kumtii kuna maana ya kuikamilisha imani yake mtu, na kwanza yeye
Imamu katakasika kutokana na kukosea na makosa.
Kumpenda Imamu ni kutimiza malipo
ya Utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Allah (s.w.t.) anasema: "...Sema
(ewe Rasuli Wetu Muhammad): kwa hayo, siombi ujira wowote kwenu ila mapenzi
(yenu) kwa watu wangu wa karibu ..."(Qur'ani, 42:23).
Imamu katakasika
kutokana na kila aina ya uchafu, uwe wa kimwili au wa kiroho. Allah (s.w)
anasema: "...Hakika Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Ahlul Bayt
(wa Rasuli Wetu Muhammad) na kukutoharisheni kwa tohara kamili" (Qur'ani
33:33).
Imamu yu mwana wa
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Allah (s.w) anasema: "...Lakini atakayekuhoji
kuhusiana na hayo baada ya kukufikia elimu, basi sema: "Njooni tuwaite
wana wetu na wana wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu na nafsi zetu na
nafsi zenu..."(Qur'ani 3:61). Mtume alitoka na Imam Hassan na Hussein (a.s)
kama watoto wake.
Imamu yu ua la Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na
anatokana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w), kama alivyosema Mtukufu Mtume (s.a.w.w)
mwenyewe, pale aliposema: "Husayn anatokana na mimi, na mimi ninatokana na
Husayn."
Imamat (Uimamu) wake
hautegemeani na upatano wa watu wala kiapo cha utii cha watu. "Yeye yu
kiongozi wa vijana wa Peponi." Yu mtakatifu (kutokana na dhambi na
kukosea) tangu kuzaliwa kwake hadi kufariki dunia kwake. Itikadi hii juu ya
Umaasum (Utakatifu wa Maimamu) ni maalumu kwa Mashia tu, na wasiokuwa Mashia
hawashiriki kwenye itikadi hii. (Ingawa wanavyuoni wakuu wasio Shia wanaweza
kuthibitisha Uma'sum wa Maimamu).
Waislamu wasio Shia, hasa wale wa
madhehebu ya Hanafii na Shafii wote, na wengi wa Hambali (Wafuasi wa Imamu
Ahmad Ibn Hambal) wanamtambua Imamu Husayn (a.s) kuwa na haki na Yazid kuwa yu
mwenye makosa. Kuzitaja rejea zote hapa kutaifanya orodha hiyo kuwa ndefu sana.
Hivyo nitazitaja baadhi tu ya rejea hizo, nilizozichagua miongoni mwa waandishi
walioandika juu ya jambo hili:
1. Allamah Shahabuddin
Abul Abbas Ahmad bin Muhammad Qastalani, aliyefariki kwenye mwaka wa 923
Hijiria, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Irshad Alsari Sharh Sahih Bukhari",
Juzuu 2, ukurasa wa 139.
2. Bwana Ibn Jawzi,
mwenye kitabu chake kiitwacho: "Al-Radd Alal Mutaassib Alanidil Man 'Min
Dhulm Yazid."
3. Bwana Sibt Ibn
Jawzi, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Tazkiratu Khawassil Ummam".
4. Allama Ibn Hajar
Al-Haitami, mwenye kitabu chake kiitwacho: As-Sawa'iq al-Muhriqah, ukurasa wa 132-134.
5. Imamu Jalaluddin
Abdul-Rahman Ibn Abi Bakr Al-Suyuti, mwenye kitabu chake kiitwacho:
"Tarikhul Khulafaa".
6. Shaikh Muhammad bin
Ali Sabban, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Is'afur Raghbiin".
7. Allama Sa'duddin
Mas'ud bin 'Umar Taftazani, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Sharh Aqaid
Nasafi".
8. Shah Abdulaziz
Dehlawi, mwenye kitabu chake kiitwacho "Sirrul Shahadatain".
9. Shah Abdulhaqq
Dehlawi, mwenye vitabu vyake "Mada-rijun Nubuwwat" na "Ja-adhbul
Qulub".
10. Maulana Abdulhai
Firangi Mahali, mwenye kitabu chake kiitwacho "Fatawi," Juzuu 3,
ukurasa wa 7.
11. Nawwab Siddiq
Hassan Khan Bhopali, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Bughyatul Raid Fi
Sharhil Aqaid".
12. Maulana Muhammad
Matin Firangi Mahali, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Wasilatun
Najat", ukurasa wa 290.
13. Mufti Muhammad
Akramuddin, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Sa'adatun Kawnain Fi Fadhailil
Hassanain."
14. Qadhi Muhammad
Sulaiman, mwenye kitabu chake kiitwacho: "Rahmatuh-Lil- 'Alamiin".
Majina haya machache ni mifano michache tu yenye kuwajumlisha wanachuoni wa
kihanafiyah, Kishafi'i na Kihambaliya ambao wameweka sehemu ya Imamu Husayn
kuwa ilikuwa ya haki na kwamba alikufa akiwa shahidi aliyedhulumiwa.
Kinyume na hivyo, wako
Mahambaliya wanaoamini kuwa Ibn Taimiya ni kiongozi wao; na hivyo ndivyo
waaminivyo Nasibi na Kharji, ambao ili kuwahadaa Masunni, hujitokeza kama
Masunni.
Watu hawa ndio siku hizi hutwa Mawahhabi, answar Sunnah na
Salafi saleh.
Watu hawa humchukulia
Yazid kuwa ni khalifa wa kweli na hivyo, Mwenyezi Mungu na atusamehe,
humchukulia Imamu Husayn (a.s) kuwa yu mwenye makosa aliyestahili kuuawa. Siku
hizi, maoni ya namna hii yanatolewa na Mahmud Ahmad Abbasi, ambaye kitabu chake
kiitwacho "Khilafat Muawiya wa Yazid" kimeziumiza hisia za Waislamu
wengi. Kwenye siku za awali, kabla ya Ibn Taimiya (aliyefariki mnamo mwaka 728
Hijiriya), mtu mmoja aliyeitwa Abu Bakr Muhammad bin Abdullah bin al-Arabi (aliyefariki
mnamo mwaka 543 Hijiriya) alijitokeza kwenye itikadi hiyo hiyo. Mtu huyo
aliandika hivi: "Husayn hakuuawa ila kwa upanga wa babu yake mwenyewe
(yaani kwa mujibu wa kanuni za shari'ah), kwa sababu alipinga kiapo cha utii
kwa Yazid na hivyo Husayn alikuwa mwasi".
Comments
Post a Comment