MAWAHHABI NA MASALAFI WAMTUKANA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).

MAWAHHABI NA MASALAFI WAMTUKANA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).
Watu hawa waliobobea kwa unafiki wamekuwa wakimtangaza Mtume wetu kuwa hukosea lakini wakidai kuwa masahaba hawakosei.
Mfano wa matusi yao kwa Mtume (s.a.w.w) ni pale wanapotafsiri aya ya surat Abasa yaani sura ya 80 humtuhumu Mtume kwa kudharau watu na kushindwa kutekeleza ujumbe wa Allah kwa ufasaha ili tu kuwalinda viongozi wao ambao ndio waliolengwa na aya za mwanzo katika surah hiyo.
Aya ya kwanza na ya pili zinasema kuwa alikunja uso na akageuka kwa sababu alijiwa na kipofu. Kosa hili wanamtupia Mtume ili kuwalinda viongozi wao.
Imepokelewa toka kwa mama wa waumini bi Aisha bint Abubakar (r.a) kuwa siku moja Mtume alikuwa katika kikao na wakubwa wa kikuraishi akiwamo: Abujahli bin Hisham, Utba bin Rabia akiwaita katika dini ya Allah. Mara akaja Abdullah bin Ummi Makhtum, ambapo Mtume ameshughulika na Maquraishi. Abdullah akamuuliza Mtume. Mtume akakunja uso na akageuka. Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha aya ya 1 na 2. Hii ndio imani ya mawahhabi.
Tazama:
Addurul Manthur J6 uk. 517
Tafsirul Qurtubi J19 uk 211
Tafsir Ibn Kathir J4 uk 502
Ona ajabu ya watu hawa wanakubali uongo huu unaohadithiwa kwa kutumia jina la Aisha ambaye alikuwa hajazaliwa. Kwa sababu imeteremkia Makkah. Kipindi hiki aidha Aisha alikuwa hajazaliwa au alikuwa mdogo sana kuweza kuhadithia tukio zito kama hili.
Lakini waislamu wa kweli (Mashia) tunaamini kuwa Mitume ni maasumu (hawafanyi dhambi). Tendo la kudharau kipofu sio miongoni mwa sifa za mitume. Ikumbukwe kuwa Allah anamsifia Mtume wake akisema kuwa ni kilele cha tabia njema (Surat Qalam).
Ukweli ni kuwa aliyekunja uso ni Uthuman bin Afan na ndiye aliyelengwa na aya hizo ili kumwonya asifanye tabia mbaya kwa kipofu tena mbele ya Mtume (s.a.ww.).
Ushahidi:
Tafsir Basair J.52 uk. 230
Tafsir Saafi J.5 uk. 284.
Almizan Fitafsiril Qur’an j.20 uk. 308
Majmaul Bayani Fitafsiril Qur’an J.5 uk. 437
Alburhan fitafsiril Qur’an J.4 uk. 427


Comments