MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Qur’an Tukufu inamtaja Mtume
Muhammad (s.a.w.), kama ifuatavyo:
“Bila shaka amekufikieni
Mtume kutoka miongoni mwenu, yanamhuzunisha yanayokutabisheni,
anakuhangaikieni, kwa waumini ni mpole, mwenye kurehemu.”(9:128)
“Nasi hatukukutuma ila uwe
rehema kwa walimwengu.” (21:107)
Huyu ndiye Mtume aliyeweza
kufanya mabadiliko makubwa duniani kuliko mtu mwingine yeyote. Wasiokuwa waislamu
wanasema yafuatayo kuhusu mtu huyu:
“Nimeumchunguza yeye (Mohammad). Ni umtu
anayevutia ajabu; na kwa maoni yangu, mbali na kuwa mpinga Kristo, ni lazima
aitwe mwokozi wa wanadamu.”
“Nina amini kwamba endapo mtu
kama huyo angeshika udikteta wa ulimwengu wa kisasa, ange fanikiwa katika kutatua
matatizo yake katika namna ambayo ingeuletea ile amani na furaha inayohitajika
hasa”
“Kama dini yoyote ingekuwa
na fursa ya kutawala uingireza, hasha, bali Ulaya nzima katika kipindi cha
miaka 100 ijayo, itakuwa ni Uislamu.”
“Siku zote nimeichukulia dini
ya Mohammad katika hadhi ya hali ya juu kwa sababu ya changamoto zake za ajabu.
Ndiyo dini pekee ambayo kwangu mimi ninaiona kuwa na uwezo wakuwiana na mabadiliko
ya kila zama za maisha ambayo inaweza kuvutia katika kila zama.”
George Barnard Shaw katika “The
Genuine Islam” Juz. 11 na. 8 (1936)
Ni maelezo mafupi ya wasifu
wa Mtukufu Mtume wa Mungu mwenye nguvu sana, Muhammad (s.a.w.), ambaye kuhusu
yeye Qur’an Tukufu inasema:
“Bila shaka amekufikieni
Mtume kutoka miongoni mwenu, yanamhuzunisha yanayokutabisheni,
anakuhangaikieni, kwa waumini ni mpole, mwenye kurehemu.”(9:128)
“Nasi hatukukutuma ila uwe
rehema kwa walimwengu.” (21:107)
Huyo ndiye mwokozi wa
ulimwengu huu, nakuombeni tumwitikie katika wito wake na tuwe waislamu wa kweli
na wapenda amani kama alivyokuwa yeye. Na wala tusiugeuze uislamu kuwa uwanja
wa vita na karaha kwa wengine kiasi kwamba ionekane kuwa kukaa na mwislamu ni
balaa.
Comments
Post a Comment