MUBAHALA KATI YA MTUME NA MAASKOFU
Muhabala ni: Kuapizana. Ujumbe wa Kikristo kutoka
Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa (a.s.). Mtume aliwajulisha
kuwa: Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam,
aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa (3:59).
Kwakuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo
wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Aya hii inaondoa dhana hiyo ambayo
inapingana na utukufu wa Mwenyezi Mungu, na inawapigia mfano wa ajabu zaidi
katika kuumbwa Adam bila ya baba wala mama. Aliumbwa kwa udongo kisha
akaambiwa: kuwa naye akawa, na kwa neno hilo hilo Nabii Isa (a.s) ndivyo
alivyoumbwa.
Ujumbe huo ulipokuwa haukukubaliana na hoja hii,
Mwenyezi Mungu akateremsha Aya:- "Na atakayehojiana nawe (Muhammad) katika
hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto
wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha
tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema
uongo" (3:61).
Hii ilikuwa
tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi, Mtume akawaita ili waanze
kuapizana. Wakajibu:- "Ngojea tujadiliane". Walipokwenda faragha,
wakamuuliza Askofu Abdul Masih; ana Maoni gani katika suala hili? Akajibu:-
Enyi Wakristo: Wallahi nyinyi mnajua kuwa Muhammad ni Nabii aliyeletwa na
amekuja na ushahidi ulio wazi juu ya jambo la huyu (Yesu a.s.). Wallahi hakuna
watu waliyeapizana na Nabii wakasalimika, ikiwa mtaapizana naye
mtaangamia". Usqufu yeye aliwaambia: "Enyi Wakristo: Mimi naziona
nyuso hizi (kundi la Mtume) kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka
mahala pake, Wallahi atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki Mkristo
ye yote hapa duniani mpaka siku ya Kiama".
Alipoulizwa Ahtam, akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza, "Ewe Abulqasim'! Unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano haya?" Mtume (s.a.w.) akamjibu: "Ninaapizana nanyi nikiwa na watu bora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu, nao ni hawa (akawaonyesha) Ali, Fatima, Hasan na Husein." Wakaogopa kuapizana na Mtume, na badala yake wakaomba sulhu kwa Mtume (s.a.w.) kwa kutoa dirham arobaini elfu.

Taz: Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 200
Tafsirul Qurtubi J.4 Uk. 104
Tafsirul Ibn Kathir J.1 Uk. 376-379
Tafsirul Khazin J.1 Uk. 359-360
Tafsirul Maragh J.3 Uk. 175
Tafsirul Kabir J.8 Uk. 81
Zadul Masir J.1 UK. 399
Katika Ayatul Mubahala, iliposema:- "Tuwaite watoto wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: Hasan na Husein. Iliposema: "Na wanawake wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: "Fatima bint Muhammad". Iliposema: "Na nafsi zetu" Mtume akamwita: "Ali". Kwa hivyo Ali bin Abi Talib ni nafsi ya Mtume Muhamad (s.a.w.).

Hii inaashiria kuwa watu bora zaidi katika Umma wa
kiislamu wote ni hao watano yaani Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Ally (a.s),
Imam Hassan bin Ally (a.s), Imam Hussein bin Ally (a.s) na bi Fatumah bint
Muhammad (a.s).
Comments
Post a Comment