NI NANI MWISLAMU?
Mwislamu ni mtu ambaye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume wake wa mwisho. Kama ukiamini haya, basi wewe ni Mwislamu.
Lakini haitoshi kusema tu kuwa mimi ni Mwislamu; bali ni wajibu juu yako kutenda kwa mujibu wa kanuni za Ki-islamu, ili uwe Mwislamu wa ukweli, na uishi duniani katika raha, na upate utukufu Akhera[1] kwa kuingia peponi na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu.
Basi ni lazima juu yako kujitahidi kufanya hayo.
Na Uislamu una sehemu tatu:
(1) Asili (Mizizi) ya Dini
(2) Matawi ya Dini (ibada mbali mbali)
(3) Tabia (Mwenendo) ya Dini
Basi anayekubali kwa ukweli Asili ya Dini, na kutumia Matawi ya dini, na akiishajipamba na tabia ya dini, basi yeye ni mbora duniani na akhera (Kiyama [2]).

Tutaendelea na somo hili insha-Alllah.
Comments
Post a Comment