SIFA ZA SHI’A
Halikadhalika, Abu’l-Muwayyid
Muwafiq Bin Ahmad Khawarizmi katika sura ya 17 ya Manaqib yake; Hakim
Abu’l-Qasim Abdullah Bin Abdullahi’l-Haskani, katika Shawahidu’t-Tanzil;
Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, uk. 119, Sibt Ibn
Jauzi katika Tadhkira, uk. 31, Munzir Bin Muhammad Bin Munzir, na hususan
Hakim, wamesimulia kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh (mmoja wa maulamaa wakubwa
wa kisunni) alisema, akitegemea juu ya ushahidi wa wasimuliaji kurudi nyuma
hadi kufikia kwa Yazid Bin Sharafi’l-Ansari, mwandishi wa Amiru’l-Mu’minin Ali
Bin Abi Talib kwamba:
Imam Ali alisema kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu
Mtume (s.a.w.w.), Mtume aliegema kwenye kifua cha Ali na akasema: “umeisikia
ile aya tukufu: ‘Wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, hao ndio bora
wa viumbe.’ (98:7)
Hawa ni Shi’a wako. Sehemu yangu
ya kukutania na wewe itakuwa ni kwenye Chemchemu ya Kauthar (katika Pepo).
Wakati viumbe wote watakapokusanyika kwa ajili ya hesabu, uso wako utang’ara,
na utatambulishwa siku hiyo kama kiongozi wa watu wenye nyuso angavu.”
Jalalud-Din Suyuti katika
Durru’l-Mansur anamnukuu Abu’l-Qasim Ali Bin Hasan (anayejulikana zaidi kama
Ibn Asakir Damishqi) ambaye anamnukuu Jabir Bin Abdullah Ansari, mmoja wa
masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema kwamba yeye na watu
wengine walikuwa wamekaa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali Bin Abi
Talib alipoingia ndani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Naapa kwa Yule
ambaye anamiliki uhai wangu kwamba mtu huyu (Ali) na wafuasi wake watapata
wokovu katika Siku ya Ufufuo.” Wakati huo huo aya hiyo hapo juu ilishushwa.
Katika sharhe hiyo hiyo, Ibn Adi
anamnukuu Ibn Abbas akisema kwamba wakati aya hiyo hapo juu iliposhuka, Mtume
akasema kumuambia Amiru’l-Mu’minin, Ali: “Wewe na waafuasi wako mtakuja Siku ya
Ufufuo katika hali ambayo kwamba wote mtaridhia juu ya Allah, na Allah
ataridhika nanyi.”
Katika Manaqib ya Khawrizmi,
ifuatayo ilisimuliwa kutoka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari: “Nilikuwa kwenye
hadhara ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoungana nasi, na wakati ule
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Huyu ambaye amekujieni ni ndugu yangu.’
Kisha, akaelekea Ka’ba, Mtume
akachukua mkono wa Ali na akasema: “Naapa kwa Yule ambaye anamiliki uhai wangu,
huyu Ali na (Mashia) wafuasi wake watakuwa wamepata wokovu katika Siku ya
Hukumu.’
Kisha akasema: ‘Ali ndiye wa
mbele zaidi yenu wote katika imani, mwenye kuzingatia mno kuhusu dhamana za
Allah, mwadilifu kupita wote katika kuamua mambo ya watu, na mwadilifu kupita
wote katika kugawa masurufu miongoni mwa watu, na aliye juu zaidi ya wote kwa
cheo mbele ya Allah.’” Katika wakati huo aya hiyo hapo juu ilishushwa.
Katika Sura ya 11 ya Kitabu
chake “Sawa’iq” Ibn Hajar anamnukuu Hafidh Jamalu’d-Din Muhammad Bin Yusuf
Zarandi Madani (Mwanachuo mkubwa wa Ahlul Sunnah) akisema kwamba: Wakati Aya
hiyo hapo juu ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali, Wewe
na Shi’a wako ndio wabora wa viumbe walioumbwa.
Wewe na Mashi’a wako mtakuja
Siku ya Hukumu katika hali ambayo nyote mkiwa mmeridhia kwa Allah, na Allah
atakuwa radhi nanyi. Maadui zako watakuwa wamechukizwa mno, na mikono yao
itakuwa imefugwa kuzunguuka shingo zao.” Kisha Ali akauliza, ni nani maadui
zangu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, “Yule ambaye ana uadui kwako na ambaye
anakutukana.”
Allama Samhudi, katika
Jawahiru’l-Iqdain, kwa idhini ya Hafidh Jamalu’d-Din Zarandi Madani na
Nuru’d-Din Ali bin Muhammad bin Ahmad Maliki Makki, ajulikanaye kama Ibn
Sabbagh, ambaye anaheshimiwa kama mmoja wa Wanachuo Mashuhuri wa kisunni na
mnadharia mkubwa wa mambo ya dini, katika kitabu chake “Fusulu’l-Muhimma”
anasimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas, kwamba wakati Aya hii iliyo kwenye
mjadala ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali; “Ni wewe
na Mashi’a wako. Wewe na wao mtakuja Siku ya Hukumu mkiwa mmefurahi mno na
mmeridhia, ambapo maadui zako watakuja na huzuni kubwa na mikono iliyofungwa.”
Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i,
mmoja wa wanachuo wenu mashuhuri katika kitabu chake “Mawaddatul’l-Qurba” na
mwanachuo anayejulikana vizuri sana kwa upinzani wake juu ya Shia, Ibn Hajar
katika kitabu chake “Sawa’iq-e-Muhriqa”, anasimulia kutoka Ummu’l- Mu’minina Umm Salma, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwamba
Mtume alisema:
“Ewe Ali,
wewe na Mashia wako mtaishi Peponi; wewe na Mashia wako mtaishi katika Pepo.”
Mwanachuo anayejulikana sana wa Khawarizm, Muwaffaq bin Ahmad, katika kitabu
chake “Manaqib” Sura ya 19, anasimulia kutoka rejea zinazoaminika kwamba
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali: “Katika umma wangu wewe ni kama
Masihi Isa Mwana wa Mariamu.”
Taarifa hii inaonyesha kwamba,
kama vile wafuasi wa Mtume Isa (A.S.) walivyogawanyika katika makundi: Waumini
wa kweli wajulikanao kama Hawari’in, Mayahudi, na wapiga chuku (wenye kutia
maneno chumvi) ambao wanamshirikisha yeye na Allah; katika njia hiyo hiyo
Waislamu watakuja kugawanyika katika makundi matatu. Mojawapo litakuwa Shi’a,
waumini wa kweli. Kundi lingine litakuwa la maadui wa Ali, na kundi la tatu
litakuwa la wenye kukuza cheo chake.
Alhamdulillah, mimi ni miongoni
mwa Mashia wa Imam Ally (a.s). Nawaomba maadui wake watubu na wajiunge nasi
katika Uislamu sahihi.
Comments
Post a Comment