UCHA MUNGU

UCHA MUNGU
"Enyi waumini, mkimcha Mwenyezi Mungu atakuongozeni njia ya haki na atawafutieni makosa yenu na atakusameheni" (8:29).
Uchamungu ni moja ya pambo lenye thamani kwa binadamu na ni kipimo cha haki na batili na kila ambacho kinamfanya mwanadamu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kwani uchamungu ni vazi zuri Ienye thamani kwa kila atakaelivaa, hupata ukunjufu wa moyo na hima ya kutafuta haki hadi kufikia kikomo na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kando ya neema zake, zikitiririka bila ya hesabu.
Katika ulimwengu huu ambao umejaa uibilisi wenye rangi tofauti, wakiwa na mitego tofauti ili kuwanasa wanadamu kwa vishawishi vipotovu na kuwatoa katika misingi ya haki na ya ukweli na yenye mwelekeo wa tawhid. Wale ambao waliofahamu hila za ibilisi na wakakana kudhalilishwa kwa kufuata vishawishi vyake, kwa hakika hawa ni katika waongofu.

Jambo la kusikitisha, ni kwamba kwa upande mwingine makafiri wana hila zao, nara zao zaweza kuwa ni uchamungu na wakafanya vitendo viovu wakiona ni vya kumridhisha Mwenyezi Mungu, hali ya kughafilika kwamba huo ni upotovu na ni chanzo cha kuangamia, lakini Mwenyezi Mungu amewaahidi wale wamchao kuwaonyesha njia ya haki.

Tuendeleze juhudi zetu katika ucha Mungu lakini tukijua kuwa Uislamu ni dini inayohimiza na kumwagiza muumini wake aishi vizuri na watu wote wanao mzunguka. Aishi nao kwa wema na awasaidie kila mara wapatapo shida bila kujadi kama ni waislamu au sio waislamu. Huu ndio ucha Mungu. 

Comments