ALAMA ZA BALEGHE KWA
MWANAMKE
Kuna baadhi ya watu ambao
wanaweza kupitiwa na miezi kadhaa tangu kubaleghe, hali ya kuwa hawalijuwi
suala hili muhimu. Na kwa wakati huo utekelezaji wa wajibu wa mambo ya kisharia utakuwa umempita katika
kipindi hicho. Hakika utambuzi wa jambo hili unahitaji kuwa makini kwa namna
Fulani, japokuwa ni jambo jepesi kwa upande wa wasichana kwani lina uhusiano na
alama tatu ambazo moja miongoni mwa hizo inatosha kuwa dalili ya kubaleghe.
Alama hizo ni hizi zifuatazo:-
1-Umri
Nao ni kutimiza miaka tisa
ya mwaka unaofuata kalenda ya mwezi mwandamo. Mwaka wa kalenda ya mwezi
mwandamo ni pungufu kwa siku kumi na saa kumi na nane ukilinganisha na mwaka
unaofuata kalenda ya Jua wa mawiyo (Grigorian callender).
2- Nywele ngumu za Sehemu ya
Siri:
Hizi ni nywele zinazodhihiri
chini ya tumbo.
3- Damu ya Mwezi:
Miongoni mwa alama za
kubaleghe, ni kupata damu ya mwezi (yaani hedhi). Na mara nyingine hupatikana
alama nyingine kama vile kuongezeka kimo, kuota matiti na kupanuka kwa uke.
Comments
Post a Comment