CHEO CHA SALMAN, ABU DHARR, MIKDADI NA AMMAR (R.A)

CHEO CHA SALMAN, ABU DHARR, MIKDADI NA AMMAR (R.A)
Assalaam alaykum:
Masunni husimulia Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isemayo: “Hakika masahaba wangu ni kama nyota; yeyote katika wao mtakayemfuata, mtakuwa mmeongozwa sawa sawa.
Abu’l-Fida anaandika katika kitabu chake cha Tarikh kwamba watu hawa wanne, ambao walikuwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijitenga, pamoja na Ali kula kiapo cha utii kwa Abu Bakar, siku ile ya Saqifa. Bila shaka kitendo cha masahaba hawa ni cha kuigwa na sisi Mashia tunawaiga wao kuupinga utawala wa Abubakar bin Quhafa.
Maulamaa wa Kisunni wameandika kwamba watu hawa wanne walipendwa na Allah na Mtume Wake. Sisi tunawafuata kama walivyomfuata Ali.
Abu Nu’aim Isfahami katika “Hilyatu’l-Auliya”, Juz. 1, uk. 172 na Ibn Hajar Makki katika hadith ya tano ya hadith arobaini zilizosimuliwa katika “Sawa’iqul- Muhriqa” kwa kumtukuza Ali, iliyosimuliwa kutoka kwa Tirmidhi, na Hakim kutoka kwa Buraida, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) alisema: “Hakika, Allah ameniamuru mimi kuwapenda watu wanne na amenijulisha kwamba Yeye mwenyewe anawapenda.”
Wakati watu walipomuuliza ni kina nani watu hao wanne, alisema: “AIi ibn Abu Talib, Abu Dharr, Mikdadi na Salman.”
Tena, Ibn Hajar katika Hadithi ya 39 amesimulia kutoka kwa Tirmidhi na Hakim kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtume amesema: “Pepo inashauku juu ya watu watatu, Ali, Ammar, na Salman.”
Je, vitendo vya Sahaba hawa Mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sio vya mfano wa kuigwa na Waislamu wengine? Je, sio aibu kwamba kwa maoni ya masunni Sahaba wamewekewa mpaka kwa wale tu waliocheza mchezo wa Saqifa, au ambao wameukubali mpango wake bila kupinga, ambapo wengine ambao wamepinga hila za Saqifa wanaonekana kama wasiokuwa waaminifu?

Hakika Masahaba hawa walikuwa wachamungu wasio tiliwa shaka hata kidogo. Na hao ni mfano mwema kwetu sisi Mashia. Hatutaki kuona dhuluma wala kwenda kinyume na maelekezo ya Allah na Mtume wake hata kidogo. 

Comments