FAIDA ZA KUUSOMA UISLAMU

FAIDA ZA KUUSOMA UISLAMU
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na rehema na amani zimshukie Mtume Wake Muhammad (SAW), Nabii wa Mwisho, na juu ya kizazi chake kitakatifu.
Hakika Umma wa Kiislamu umeshindwa kabisa, na kushindwa huko kunafuatia machungu na mateso; kisha ukosefu mkubwa katika pande mbili: upande wa kimaada (kidunia) na upande wa kimaanawi (kiroho). Kukosekana upande wa kimaanawi ni sababu ya kukosekana upande wa kimaada, kwani umaada sio nguvu inayojileta yenyewe kwa mtu na kuweza kubaki au kuondoka wakati wowote, bali ni natija ya kazi ya mtu na mapato ya juhudi yake. Mtu hafanyi bidii ila baada ya kujua maana ya juhudi yake.
Kwa hivyo, kukosekana umaanawi katika Umma wa Kiislamu ndiko ambako kunapasa kuupiga vita na kuupigania ili urudi utukufu na ushindi na Umma uishi katika neema baada ya kuwa katika adhabu. Hatuwezi kuupiga vita ukosefu huu bila ya kueneza mwamko sahihi wa Kiislamu kwa kutafsiri Qur'ani, kueneza maarifa yake. Kuelezea maisha ya mashujaa wa Kiislamu.
Hii ndio sababu iliyonifanya nitumia muda wangu kuandaa mada mbali mbali na kuziingiza katika mtandao ili ndugu zangu waislamu na wale wasiokuwa waislamu wasome na waelewe maanawiya ya kiislamu. Uislamu ukieleweka vizuri, tutapata maendeleo na nchi yetu itakuwa na amani tele.

Comments