HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI
Mwenyezi Mungu Mwenye Rehma amesema katika Qur’ani tukufu kuwa: “Akasema: Hakika wafalme wanapouingia mji,  wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili; hivyo ndivyo wanavyofanya”. (27:34)

Aya hii inatoa ujumbe kwa Waislamu ulio muhimu sana. Inaeleza kwamba unapotokea ufalme usiotosheka  na milki yake na ukawa na nia ya kutaka kupanua  himaya yake na mipaka yake, basi daima ufalme kama huu hauwezi kuzingatia kanuni za haki katika  nidhamu yake. Na hapo ufalme huo hupotoka na kuanza kuvamia nchi nyingine na kuiteka miji yake na kufanya ufisadi ikiwa ni pamoja na kuharibu mali na kuhilikisha maisha ya wanadamu. Kwa kuwa  Mawahhabi historia yao inaonyesha kutokana kwao  na mambo ya ufalme na mauaji hapana shaka kuwa aya hii inazungumzika katika fitna yao. 

Comments