MAANA YA MAWAHHABIYA

MAANA YA MAWAHHABIYA
Kwa kufuatana na maelezo ya wanachuoni waliochimbua Historia ya Wahhabi, neno “Wahhabi” limetokana na jina la Abdul Wahhab ambalo ni jina la baba wa Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhab.

Wale watu wanaofuata itikadi potofu ya Sheikh Muhammad ndio hao wanaoitwa  “Wahhabi”. Wanachuoni wengi walichagua wafuasi hawa wa itikadi potofu waitwe kwa lakabu hiyo kwa sababu wanaona kwamba isingewezekana kuitwa “Muhammadiya” sawa na jina la Sheikh wao kwa kuwa jina hilo ni la Mtukufu Mtume (s.a.w.).  Isingekuwa vyema watu wapotofu na mafisadi kama hawa wanaopotosha mafuzo yake wachukue jina lake kuwa anuani ya uharibifu wao. Na vile vile mara nyingi  wanachuoni hujulikana kwa lakabu zao. Mfano ni  huu: Ibn Jauz, Ibn Nabati, Ibn Kathiir, Ibn Jarir, Ibn Maja, Ibn Sina, Ibn Qayyim, Ibn Askary n.k. Na yeye Sheikh Muhammad akaitwa Ibn Abdul Wahhab. 

Comments