MAELEZO YA IMAM IMAM JAAFAR SWADIQ KUHUSU MWANADAMU
"Allah (s.w.t.)
alikuwepo kabla hakujakuwa na kitu chochote na atakuwepo kiroho kupindukia
milele. Atukuzwe Yeye kwa vile Ameufanya ufunuo wake kwetu. Kwake Yeye
Anastahiki shukurani zetu za dhati kwa sababu ya tunu yake kwetu.
Allah Ametupa sisi
daraja kubwa pamoja na elimu bora na akatuanisha sisi pamoja na utukufu wa cheo
(kwani kwa vile tu) kizazi cha Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) kupita viumbe
vyote kwa elimu yake, ikiwa ni dhamana tukufu, pamoja nasi ya upambanuzi wa
(mambo) ya ulimwengu huu.
Wababaishaji
wameshindwa kufahamu siri na sababu zilizo msingi wa asili ya viumbe, na akili
zao zimebaki kutokuwa na habari ya ustadi usio na kosa uendeleao kuwepo chini
ya uumbaji wa jamii mbali mbali (za viumbe) wa bahari na bara, tambarare na
miinuko miinuko.
Wakawa makafiri, na
kwa sababu ya kasoro ya elimu yao na ufinyu wa akili, wakaanza ulaghai
ushindanao pamoja na ukweli, kiasi kwamba waliukataa uumbaji na kudai kwamba
ulimwengu wote huu hauna maana yoyote ni bure tu, bila kuwa na ustadi wowote wa
usanii juu ya uhusikaji na usanii au Muumba - bila kusudio usio na mwisho bila
uwiyano au utulivu.
Allah (s.w.t) yu
mbali mno na yale yote wanayomhusisha nayo. Na wapotelee mbali! Kulioje
Kupotoka kwao! katika upofu wao wa kupotoka na bumbuazi, wako kama watu vipofu
wapapasao kulia na kushoto katika nyumba iliyopambwa vizuri, iliyojengwa vizuri
pamoja na mabusati mazuri, vitu vitamu vya chakula na vinywaji, aina mbalimbali
za nguo na vitu vingine muhimu vya matumizi ya lazima, vyote vimewekwa kwa
kutosheleza kwa kiasi kizuri na kuwekwa kwa ukamilifu makini na ustadi wa
kusanii. Katika upofu wao wameshindwa kuliona jengo hilo na mapambo yake.
Wanapita kutoka chumba kimoja kwenda kingine, wakiendelea mbele na kurudi
nyuma. Kama kwa bahati yeyote mmoja kati yao atakuta kitu chochote katika
mahali pake kinatoa hitaji, na asijue kusudio la kuwekwa pale na asijue
(usitajwe) ustadi ulio chini yake, huenda akaanza kumlaumu Mjenzi wa (hilo)
jengo kwa chuki zake na hasira, wakati ambapo, kusema kweli, makosa ni yake kwa
kutokuwa na uwezo wa kuona.
Kutokulingana huku
kwa tabia hushikilia vizuri katika kadhia ya tapo, ambalo hukataa nguvu iumbayo
na hoja hiyo ipendeleayo usanii wa Kiungu. Hushindwa kutambua ubora wa riziki
zao, ukamilifu wa uumbaji na uzuri wa Usanii, wanaanza kutangatanga katika
mapana ya dunia, wakifadhaishwa kwa kutokuweza kwao kufahamu kwa akili zao
sababu na misingi iliyo chini yake. Hutokea hivyo wakati mwingine kwamba mmoja
miongoni mwao anayo habari ya kitu, lakini katika ujinga wake juu ya ukweli
wake, kusudio na mtaji, huanza mara moja kulitafutia kosa akisema, "Ni
kosa lisilothibitika."
Wafuasi wa Mani (Mtu
aliyeanzisha Dhehebu la Zorasti wakati wa Mfalme Shapur mwana wa Urdisher,
ambaye aliamini Utume wa Isa (a.s.) lakini akaukataa ule wa Musa (a.s.) na
ambaye aliamini katika Uwili wa Uungu kama Waumbaji wa vizuri vyote na viovu
katika ulimwengu huu - Nuru moja kama Muumba wa vitu vizuri, nyingine ya giza,
kama ile ya wanyama wakali na viumbe vyenye madhara) ambao, kama valivyo
washupavu katika kundi potovu la uovu, wameanza kutangaza waziwazi upotofu wao.
Mbali na haya, baadhi ya watu wengine ambao waliopotoka nao pia wamepotea
kutoka fadhila za Kiroho (Kiungu) kwa kutamka tu kama yakini halisi
isiyothibitika au isiyowezekana.
Inampasa mtu ambaye
Allah (s.w.t.) amemjaliya elimu ya maajabu ya Kiroho ya ukweli na ambaye
amemuongoza kwenye imani yake, na ambaye amepewa kuona na kutafakari juu ya
ujuzi wa usanii ulio chini ya uumbaji, na ambaye ametunukiwa uelezaji wa sifa za
vitu hivyo, juu ya msingi wa akili isadikishayo na sifa nzuri. Inampasa mtu
kama huyo kumtukuza Allah (s.w.t.) kwa ukamilifu kama Mola wake na fadhila za
Kimbinguni, na kumuomba Yeye kwa kumzidishia elimu ya mambo ya Kiroho na
msimamo imara ndani yake, na uwezo wa juu wa maelezo juu ya hayo.
Allah (s.w.t.) asema,
"Nitaongeza fadhila zangu, kama mtakuwa ni wenye kushukuru, na adhabu
yangu ni kali kama hamtakuwa wenye kushukuru."
Muundo wa Ulimwengu
huu ni mwongozo wa juu zaidi na hoja ya kuwepo Allah (s.w.t.) - jinsi sehemu
zake (huo ulimwengu) zilivyounganishwa pamoja na kuwa na ufundi mzuri wa
Usanii.
Hali ya kufaa
kutafakari na akili kuangalia kuhusu sehemu moja moja hudhihirisha kwamba
ulimwengu huu unalinganishwa na nyumba iliyopambwa na vitu vyote muhimu kwa
ajili ya mwanadamu.
Mbingu hii ni kama
chandalua; ardhi imetandazwa kama busati ambapo nyota zimewekwa katika safu juu
ya safu zikijitokeza kama taa zilizowashwa katika sehemu zao. Vito vya thamani
vimehifadhiwa kama kwamba ni nyumba yenye mkusanyo wa vitu vingi. Mbali na hivi
kila kitu kiko tayari kupatikana kukidhi mahitaji ya mtu binafsi.
Mtu, katika Ulimwengu
huu, ni kama bwana mmiliki mwenye nyumba, akiwa ni mwenye kumiliki kila kitu
ndani yake.
Na siyo jamii tofauti
za mimea zipatikanazo kukidhi mahitaji ya mtu binafsi - baadhi ni chakula cha
wanyama, nyingine ni dawa kwa Wanadamu; baadhi ni kwa mapambo tu, baadhi ni
kumpatia mtu manukato kwa burdani yake, baadhi ni dawa kwa wanyama, baadhi ni
lishe kwa Mwanadamu, baadhi kwa ndege tu na nyingine kwa wanyama wa miguu minne
peke yao na kuendelea. Jamii tofauti za wanyama zimepangiwa kazi kwa mahitaji
na faida maalum.
Comments
Post a Comment