Bismillahir Rahmanir
Rahiim. Dokezo Na wanasema: Hatoingia peponi ila aliyekuwa myahudi au mkristo,
Hayo ni matamanio yenu! Sema leteni Hoja zenu ikiwa mnasema kweli(2:111). Ama
yule aliyeanzisha viumbe, kisha atavirudisha, na anayekuruzukuni toka mbinguni
na ardhini (siye Mweza?). Je, yuko Mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: "Leteni ushahidi (jengeni hoja)
wenu wa kuthibitisha ikiwa mnasema kweli!"(27:64).
Maana ya mantiki. Kwa
mujibu wa aya tulizozinukuu, mantiki ni utaratibu mzuri wa kufikiri*. Ni fani
ya elimu inayojishughulisha na utoaji wa hoja. Na kwa kuwa kutoa hoja ni
kufikiri, twaweza kusema kuwa mantiki ni taaluma inayojihusisha na kufikiria
juu ya kufikiri. Kutoa hoja: Kutoa hoja ni kutumia ukweli unaojulikana ili
kuthibisha ukweli mwingine au kuonyesha uongo wa jambo. Kwa maneno mengine,
kutoa hoja ni kutafuta ushahidi uliodhahiri wa kuthibitisha ukweli au kuonyesha
uongo wa jambo.
Mfano Katika Biblia, Mtume Paulo ambaye ni mwanzilishi wa Imani ya kudai kuwa "Yesu ni Mungu" anasema hivi: "Tukilitizamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa kristo Yesu, Mungu mkuu na mwokozi wetu".
Ninenalo silineni agizo Bwana, bali kama kwa upumbavu katika ujasiri huu wa kujisifu* Lakini Yesu Mwenyewe anasema hivi: Na uzima wa milele ndiyo huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Ama, Paulo atakuwa kaongopa au Bwana Yesu atakuwa kasema kweli. Paulo anakiri kuwa haneni agizo la Bwana, kwahiyo atakuwa kaongopa kusema,Yesu ni Mungu Mkuu.
Mfano wa Hoja: Yesu kazaliwa, na kila azaliwaye ni kiumbe, kwa hiyo Yesu ni kiumbe. Mbuzi ni mamalia, mamalia wote hunyonyesha watoto wao, kwahiyo mbuzi hunyonyesha watoto wao. Kama kusema 'Yesu si Mungu' ni kosa, Dibagula alistahiki kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini Dibagula kaachiwa huru, kwa hiyo kusema 'Yesu si Mungu' si kosa! Hakika mfano wa Yesu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adamu, alimuumba kwa udongo kisha akasema: "Kuwa!" basi akawa. ( Qur’an 3: 59). Kufikiri kimantiki: Kufikiri kimantiki ni kufikiri kwa kutoa hoja. Ni kutafuta ukweli/ushahidi uliodhahiri wa kuthibitisha ukweli au kuonyesha uongo wa jambo.
Comments
Post a Comment