MAWAHHABI NA MASALAFI WAWAPORA NA KUWAUA WAISLAMU
WA TA’IF
Wakati Maulamaa wa Ahl as-Sunna
walipowanyamazisha Mawahhabi katika mwaka 1210 A.H. (1796), Maulamaa wa Makkah
walitayarisha waraka na kutia sahihi zao ambamo waliandika Ayah za Qur’an
Tukufu pamoja na Hadith sharif kwa kuthibitisha kuwa Uwahhabi ni njia iliyo
tofauti na mbali na Islam, mtego wa hila na njama zilizotengenezwa na maadui wa
Islam kwa ajili ya kuuteketeza Uislam undani mwake. Nakala za azimio hilo
zilitumwa katika nchi zote za Kiislamu.
Baadhi ya Mawahhabi wa Makkah
walimwendea ‘Abd al-‘Aziz, mtawala huko Darr’iyya, na kumwelezea kuwa
wawakilishi wao hawakuweza kuwakabili Maulamaa wa Makkah na kwamba waraka wa
azimio lao kuwa Uwahhabi ulikuwa ni upotofu na njama dhidi ya Islam,
zimepelekwa kila nchi ya Kiislam. ‘Abd al-‘Aziz ibn Muhammad ibn Sa’ud na
wafuasi wake, waliingiwa na hasira kali kabisa dhidi ya Ahl as-Sunna,
waliishambulia Makkah katika mwaka 1215. Amir wa Makkah, Sharif Ghalib ibn
Musa’id ibn Sa’id Effendi, aliwakabili vikali. Damu nyingi ilimwagika pande
zote mbili. Sharif Ghalib Effendi hakuwaruhusu hao kuingia Makka, lakini
makabila ya Waarabu kuzunguka Makkah walikubali Uwahhabi. Baina ya Idi mbili za
mwaka huo huo, Sa’ud alituma jeshi katika mji wa Ta’if. Huko wao waliwatesa na
kuwachinja ovyo Waislamu wanawake na watoto wa Ta’if.
Mateso na mauaji ya Ta’if wakiwemo
wanawake na watoto yalifanyika kwa amri ya adui mkubwa wa Islam, brigadia mwovu
kabisa aliyekuwa akiitwa ‘Uthman al-Mudayiqi. Mtu huyu na Muhsin walikuwa
wametumwa na Sharif Effendi kwenda Dar’iyya ambapo walitakiwa kuzungumzia
mapatano ya awali ya kuwazuia Mawahhabi wasiizingire Madina na kutowatesa
Waislamu. Lakini mnafiki huyu alikuwa ni jasusi kwa Sharif Effendi.Yeye
alimhadaa mwenzake Muhsin, wakati wanaelekea Dar’iyya kuwa angeliweza kumpatia
mafanikio mengi.
Hao wawili walitoboa siri zao kwa
Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz huko Dar’iyya. Sa’ud, alipowatambua kuwa wao walikuwa
watumwa wake watiifu, aliwaweka waporaji chini ya ukamanda wao. Wao walikwenda
hadi mahala paitwapo Abila karibu na Ta’if na huko wakampelekea Sharif Ghalib
Effendi barua kuwa Sa’ud na wao, wasaliti hao wawili, walikuwa hawatambui
uhalali wa mapatano ya hapo awali na kwamba Sa’ud alikuwa akijitayarisha
kuuzingira mji wa Makka.
Sharif Ghalib Effendi aliwajibu
katika lugha laini akiwashauri, lakini ‘Uthman mkatili, alikuwa kwa hakika adui
mkubwa wa Islam, alizichana barua. Yeye aliwashambulia Waislamu waliokuwa wametumwa
na Amir na kuwaghalibu. Ilimbidi Sharif Ghalib Effendi alirudi hadi ngome ya
Ta’if na kuchukua hatua za kujihami. Huyu Muwahhabi katili aliweka kambi za
majeshi yake huko Malis karibu na Ta’if mwishoni mwa mwezi wa Shawwal katika
mwaka 1217 A.H. (1802). Yeye vile vile alioomba msaada kutoka mkatili Amir wa
Bisha, Salim ibn Shakban, ambaye alikuwa na roho katili kuliko jiwe lililojaa
uadui dhidi ya Uislamu. Kulikuwapo na tawala za kifalme takriban ishirini
katika majangwa na kila falme alikuwa na kikosi cha Mawahhabi mia tano zaidi ya
kikosi cha Salim mwenyewe kipatacho elfu moja.
Wakazi wa Ta’if wakiongozwa na
Sharif Ghalib Effendi, waliwashambulia majeshi ya Mawahhabi huko Malis.
Alifanikiwa kuwaua waporaji elfu moja na mia tano wa Salim ibn Shabkan. Salim
pamoja na wafuasi wake walitoroka Malis. Lakini walikusanyika na wengine na
kurejea kuishambulia Malis na waliupora mji mzima.
Sharif Ghalib Effendi alikwenda
Jeddah kutafuta msaada wa kijeshi. Wakazi wengi wa Ta’if walikuwa wamejaa kwa
khofu na walitoroka kwa kisiri siri pamoja na vitu vyao vya majumbani. Ingawaje
wale wakazi wa Ta’if waliokuwa wamejisitiri katika ngome, waliweza kuwashinda
majeshi madogo madogo ya Mawahhabi waliokuwa wakijaribu kuwashambulia, wao
walipeperusha bendera nyeupe ya kutaka usitishwaji wa vita baina yao kwani
Mawahhabi walikuwa wakimiminika majeshi mengi. Wao walikubali kujisalimisha kwa
masharti kwamba maisha na heshima zao hazitadhuriwa.
Ingawaje maadui pia walikuwa
wamekwisha nguvu na kudhoofika kwani nao pia walipata pigo kubwa la kuuawa na
wengi walitoroka kutoka majeshi yao na walidhoofika pia, akatokea mwakilishi wa
wakazi wa Ta’if, ambaye alikuwa mwovu na msaliti mkubwa, ingawaje alikuwa
akiwaona Mawahhabi wanatoroka kwa kukimbia hapo, aliwapigia sauti kubwa kwa kuwaambia,
“Sharif Ghalib ametukimbia kwa kuogopa! Na hivyo wana-Ta’if hawana nguvu ya
kukabiliana nanyi! Wao wamenituma kuwaleteeni habarri kuwa wao wapo tayari
kujisalimisha na kuisalimisha ngome nzima mikononi mwenu na wanawaombeni
muwasamehe. Mimi ninawapenda Mawahhabi. tafadhalini rudini! Nyinyi mumemwaga
damu nyingi kupita kiasi na haitakuwa jambo la busra kwenu nyinyi kurudi bila
ya kuikamata Ta’if. Ninaapa kuwa wana-Ta’if watajisalimisha wao na ngome hiyo.
Wao watakubalia chochote kile mutakacho nyinyi.” Kwa hakika lilikuwa ni kosa la
Sharif Ghalib Effendi katika kuipoteza Ta’if bila maana. Iwapo angalikuwa
amebakia Ta’if pamoja na Waislamu, basi isingalifika maafa hayoo. Kwa sababu
waporaji ni waoga, Mawahhabi hawakudhani kuwa wana-Ta’if watajisalimisha vile
kirahisi.
Lakini walipoona bendera ya kutaka
amani juu ya ngome, walimtuma jasusi kuja kujua hali halisi iliyokuwapo ndani
mwa ngome. Wana-Ta’if walimvuta ndani kwa kamba huyo mjumbe. Mjumbe huyo
aliwaambia: “Kusanyeni mali zenu zote hapa na mujisalimishe kama munataka
kuishi hai.” Mali zao zote zilikusanywa na kurundikwa mahala pamoja kwa msaada
wa Mwislamu mmoja aliyekuwa akiitwa Ibrahim. Mjumbe huyo alisema: “kwa hakika
hii haitoshi.” Aliendelea kusema kuwa “Sisi kamwe hatuwezi kuwasameheni kwa haya
tu, lazima mulete zaidi na zaidi!” Yeye aliwapa daftari na kuwaambia
“orodhesheni majina ya wale wanaokataa kutoa mali zao! Wanaume wapo huru kwenda
popote pale watakapo isipokuwa wanawake na watoto watafungwa kwa minyororo.”
Kwa hakika wote kwa pamoja walimwomba awe mlaini mwenye huruma kidogo, basi
yeye aliongeza udhalimu na uovu wake.
Ibrahim, alishindwa kuvumilia zaidi
ya hapo na hivyo alimpiga kifuani kwa jiwe na kumwua. Wakati malumbano haya
yanaendelea, Mawahhabi waliishambulia na ngome hiyo na hivyo waliweza kukwepa
kulengwa mizinga na risasi. Wao walibomoa milango na kufanikiwa katika kuingia
ndani ya ngome. Mawahhabi waliwaua wanawake, wanaume na watoto wote waliowaona
na hata kuthubutu kuwaua watoto wachanga waliokuwa katika masusu yao. Mitaa ya
mji ilijaa kwa mito ya damu. Wao walishambulia kila nyumba na kupora vyote
vilivyokuwamo na popte pale walichokipata, wakawa wakishambulia kama vichaa na
kikatili hadi usiku ulipoingia. Wao hawakuweza kuzichukua nyumba za mawe upande
wa mashariki wa ngone, hivyo walizishambulia nyumba hizo kwa risasi. Mlaghai
moja wa Kiwahhabi alipiga kelele: “Sisi tunawasameheni! Munaweza kwenda popote
pale mupendapo pamoja na wake na watoto wenu,” lakini wao waliyapuuzia bila
kujali. Wakati huo Mawahhabi waliwakusanya watu, ambao walikuwa wakijitayarisha
kuondoka na kuhama, juu ya mlima na kuzizunguka zile familia halisi za
Waislamu, ambao wamekua katika mapenzi na udugu na wengi wao walikuwa ni
wanawake na watoto, na kuwaweka wakafa kwa njaa na kiu kwa muda wa siku saba,
na kuwatesa mno kwa visingizio, kupiga mawe na vitisho vya aina mbalimbali.
Mawahhabi walimwita mmoja baada ya
mwingine na kuwapiga na kuwauliza: “Tuambieni pale mulipoficha mali zenu!” na
walipiga makelele, “Siku yenu ya kufa inawadia!” kwa wale walioomba msamaha.
Ibn Shakban, baada ya kuyakandamiza
majumba hayo ya mawe kwa muda wa siku kumi na mbili bila ya kufanikiwa
kuyabonyeza, aliahidi kuwa wale wote watakaotoka nje ya nyumba zao na
kujisalimisha pamoja na silaha zao, basi watasamehewa. Kwa hayo, Waislamu
walimwamini na kutoka nje, lakini, wakiwa wamefungwa mikono yao migongoni mwao,
wao waliburutwa na Ibn Shakban hadi juu ya mlima pale ambapo walikuwapo
Waislamu wengine waliokuwa wameshikiliwa. Waislamu mia tatu na sitini na saba,
wakiwemo wanaume, wanawake na watoto (Allah swt awarehemu) wote kwa pamoja
walichinjwa chinjwa mlimani hapo.
Mawahhabi waliwaachia wanyama wao
wawakanyage Waislamu hao na hatimaye kuwaacha hapo bila ya kuwazika ili waliwe
na ndege wa kuwinda kwa muda wa siku kumi na sita. Wao walifanya hujuma kubwa
ya kupora mali za Waislamu katika kila nyumba, na waliweza kukusanya mali
nyingi mno mpaka kukutokea kama mlima mbele ya lango la ngome hiyo na
walimtumia Sa’ud asilimia ishirini ya yale yaliyoporwa na iliyobakia waligawana
miongoni mwao. Wadhalimu na mvua za masika zilizoa mapesa na vito vya thamani
mno na hapo kulibakia kiasi cha rial za dhahabu elfu arobaini tu, katika mikono
ya Ahl as-Sunna; kiasi cha rial elfu kumi ziligawiwa miongoni mwa wanawake na
watoto, na vitu viliuzwa kwa bei ndogo kabisa.
Mawahhabi walizichana nakala za
Qur’an tukufu na vitabu vya tafsir, Hadith na vitabu mbalimbali vya Kiislamu
walivyovichukua kutoka maktaba, misikiti na majumbani mwa watu, na kuvitupa
huku na huko. Wao walithubutu hata kutengenezea viatu kwa ajili miguu yao
michafu vya majalada ya dhahabu ya Qur’an na vitabu vinginevyo. Kwa hakika
zilikuwapo zimeandikwa Ayah tukufu za Qur’an juu ya majalada hayo.
Majani (makurasa) ya Qur’an tukufu
zilikuwa zimetupwa ovyo mitaani mwa mji wa Ta’if kiasi kwamba kulikuwa hakuna
hata nafasi ya kuuweka mguu juu ya ardhi ya mji wa Ta’if. Ingawaje inasemekana
kuwa Ibn Shakban alikuwa ametoa amri ya kutokuzichana nakala za Qur’an Tukufu,
lakini hao Mawahhabi waporaji wa majangwani hawakujua Qur’an ni nini, na hivyo
walizichana chana nakala zote walizozipata na kuzikanyaga kanyaga ovyo.
Inajulikana kuwa ni nakala tatu tu za Qur’an Tukufu na nakala moja tu ya Sahih
al-Bukhari ndizo zilizo salimika kutokana na hujuma na uporaji wa Mawahhabi
katika mji mkubwa wa Ta’if.
Comments
Post a Comment