NAMNA YA KUTAWADHA
Kabla ya kuswali ni lazima utawadhe {ufanye Wudhu}.
Na namna ya kutawadha ni kama ifuatavyo:-
{a} Chukua maji mataharifu na ya halali, na viwe viungo vyako ni
tohara.
{b} Kosha mikono yako viganjani mara tatu.
{c} Sukutuwa na utie maji puwani, kila kimoja mara tatu.
{d} Kisha kusudia kuwa "Mimi ninatawadha kwa kutaka ukaribu
wa Mungu.
{e} Osha usoni kwako, kuanzia maoteo ya nywele za kichwa. na
utakosha mpaka kidevuni, ndio urefu na ukati wa dole gumba na kidole cha
shahada, ndio upana wa uso.
{f} Baadae utakosha mkono wa kulia, kuanzia juu ya kisigino, mpaka
nchani mwa vidole.
{g}Kisha utaosha mkono wa kushoto vilevile.
{h} Kisha utapaka kwa kiganja chako cha kulia sehemu ya mbele ya
kichwa.
{i}Baadae utapaka kwa mkono wako wa kulia juu ya mgongo wa unyayo
wako wa kulia, kuanzia vidoleni mpaka katika kifundo.
{j} Baadae utapaka kwa mkono wako wa kushoto juu ya mgongo wa
unyayo wa kushoto vilevile.
Hapo udhu tayari na unakuwa tayari kwa ibada. Utaratibu huu ni kwa
mujibu wa Qur’an na sunnah za Mtume Muhammad (s.a.w.w). Tofauti na hivi ni
utaratibu uliobuniwa baadaye na watawala waliowatawala waislamu kwa mabavu na
ninaweza kudiriki kusema kuwa ni bid’a.
Hala hala, tunapoipata Sunnah moja tuitekeleze mara moja na
tunaifahamu bid’a moja tuachane nayo mara moja hata kama tumezoea kuifanya,
insha-Allah.
Comments
Post a Comment