NI NANI BIN ABDUL WAHHAB
Yeye ni Muhammad bin Abdul
Wahhab bin Sulayman bin Ally bin Muhammad bin Ahmed bin Rashid wa kabila la
Banu Tamim. Alizaliwa mnamo mwaka 1115 A.H. (1703 A.D) katika mji wa Uyayna, katika
nchi ya Najd iliyoko mashariki ya nchi ya Hijaz (nchi yenye miji ya Maka na
Madina).
Kuna hadithi nyingi za Mtume (s.a.w.) zinazowazindua Waislamu juu
ya fitna na balaa la utovu litakalotokea katika dini kwa kuletwa na watu kutoka
Najd. Wanachuoni wengi wamehakikisha
kuwa hadithi hizo zilikuwa zikimtabiri Muhammad bin Abdul Wahhab, na wazushi
wengine waliotokea mapema kama vile Musaylimah al-Kadhdhaab, ambaye ni babu
wamababu wa Mfalme Muhammad bin Saud aliyeasisi Saudi Arabia kwa kushirikiana na Muhammad bin Abdul Wahhab na
kwa msaada mkubwa wa Serikali ya Uingereza.
Katika hadithi mojawapo ambayo Mtukufu Mtume
(s.a.w.) anamtabiri Muhammad bin Abdul
Wahhab alisema: “Atakuja tokea Shetani kutoka (mji wa) Najd, atatia msukosuko (mtikisiko) katika kisiwa (eneo)
cha Arabuni kutokana na fitna yake”. (al-Fajr S’adiq uk.21)
Katika hadithi nyingine
Mtume (s.a.w.) amesema: “Itatokea fitna kutoka huko”; huku akiashiria kwa mkono wake mtukufu upande wa mashariki (yaani
Najd).
Nchi ya Najd ndiyo ambayo
Muhammad bin Abdul Wahhab alizaliwa. Na ndio nchi hiyo hiyo ambayo Mtume wa
Mwenyezi Mungu alikataa kuiombea dua wakati alipofikiwa na wageni kutoka katika
mji huo. Na hadithi inayozunguzia habari hiyo si tu kwamba ni mashuhuri bali imenakiliwa pia na Wahhabi wenyewe katika kitabu chao juu ya maisha ya
Sheikh wao Muhammad bin Abdul Wahhab ambacho
kilichapishwa kwa idhini ya Mfalme Faisal. Jina la kitabu hicho ni
“Sheikh Muhammad bin Abdul Wahhab”.
Katika kitabu hicho uk. 86 imenakiliwa
hadithi hiyo ambayo Mtume katika dua yake aliweka wazi ubaya wa watu
watakaotoka Najd juu ya Uislamu.
Mtume (s.a.w.) alikuwa
akiomba akisema:
“‘Ewe Mola wangu! Tubarikie sisi katika Shamu
na Yemen’. Wakasema (Watu wa Najd): ‘iombee na Najd yetu Ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu’. (Mtume) akakariri dua hiyo mara
tatu akiiombea Shamu na Yemen na hali wao (watu wa Najd) wakisema iombee na
Najd yetu Ee Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Mara ya nne (akajibu) akasema: ‘Huko
(Najd siombei) ni mahala pa misukosuko na fitna’”.
Hadithi zote hizo zinaelezea
jambo moja tu, nalo ni kutokea fitna kutoka Najd. Kwa kutaka kutimiza ukweli wa maneno ya Mtume wake (s.a.w.),
Mwenyezi Mungu akauhakikisha usemi huu
wa Mtume (s.a.w.). Akatokea Muhammad bin Abdul Wahhab, akaungana na Muhammad bin Saud kwa tamaa ya
mali na utukufu wa ufalme, na kutoridhika na milki yake ya Najd, wakazivamia
ardhi za Hijaz; wakamwaga damu kwa kiasi
cha kutisha kwa ukatili mkubwa kabisa na
bila kujali watoto wadogo, vikongwe,
wanawake na watu kadhaa wasio kuwa na hatia yoyote. Matendo yao mabaya ni pamoja na kupora mali
za watu, ikiwa ni pamoja na kuwakufurisha Waislamu waaminio na kuwalinganisha na wapagani wa
Makka waliokuwa wakiabudu masanamu; hali
ya kuwa Waislamu wale walikuwa
wakimpwekesha Mwenyezi Mungu.
Kwa kifupi, katika vitabu
vya historia Muhammad bin Abdul Wahhab
amejulikana kama “Shaikh an-Najd”. Jina hili linakamilisha utabiri wa Mtume
(s.a.w.) juu ya kutokea Sheitani kutoka Najd.
Kwani wanavyuoni wa Fiqhi
(wanasheria wa Kiislamu) wanaposema “Shaikh an-Najd” huwa wanamkusudia Iblisi
na ukisoma hadithi ile ya mwanzo utaona Mtume (s.a.w.) anasema “Atatokea
Shetani kutoka Najd”. Basi hapana shaka kuwa aliyetajwa hapa ni Muhammad bin
Abdul Wahhab. Basi namna gani Waislamu wanaweza kumfanya mtu aliyetajwa na
kuitwa Shetani na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa Imam wao?
Comments
Post a Comment