SABABU ZA WA-IRANI KUUPOKEA USHI’A

SABABU ZA WA-IRANI KUUPOKEA USHI’A.
Wanafiki hudai kuwa, “Ushia ni Dini ya kisiasa, na kwamba Mazoroasta wa Iran wameukubali kwa ajili ya kujiokoa kutoka umiliki wa Waarabu, wamesema hivyo katika upofu wa kufuata watangulizi wao. Nimekwishathibitisha kwamba ni dini ya Uislamu, dini ambayo Mtume (s.a.w.w.) ameiweka amana mikononi mwa wafuasi wake. Kwa kweli, wale ambao bila kibali chochote kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), wakaweka msingi wa Saqifa, walikuwa ndio wenyewe wanasiasa na sio wafuasi wa familia Tukufu ya Mtume (s.a.w.w.).
Ni tabia ya Wa-Iran kwamba wao hutazama mambo kwa kuyachunguza. Wakati watakaposadikishwa na ukweli wake, wanayakubali, kama ambavyo waliukubali Uislamu wakati Iran iliposhindwa na Waarabu. Hawakulazimishwa kufanya hivyo. Waliuacha Uzoroasti na kwa uaminifu kabisa wakaushika Uislamu.
Halikadhalika, wakati waliporidhishwa na mantiq na huduma za Ali zenye thamani isiokadirika, wakaukubali Ushi’a. Kinyume na maelezo ya waandishi wa kiwahhabi na kisalafi,Wairani hawakumkubali Ali wakati wa Ukhalifa wa Harun-r-Rashid au Maamunu’r-Rashid.
Walimkubali Ali wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Salman Farsi alikuwa mmoja wa wafuasi waaminifu kabisa wa Imam Ali (a.s). Alifikia kiwango cha juu cha Imani. Maulamaa wa Madhehebu zote kwa makubaliano ya pamoja wameandika kwamba Mtume amesema: “Salman anatokana na Ahlul Bait wetu (yaani ni mmoja wa watu wa Nyumba yangu).” Kwa sababu hii aliitwa “Salman Muhammad” na yeye inakubalika kabisa kuwa ni mfuasi thabiti mwenye kumuunga mkono imam Ali, na mpinzani mkali wa Saqifa.
Kama, kutegemeana na vitabu vya kisunni, sisi tukimfuata yeye, basi tuko katika njia iliyonyooka. Alizisikia aya za Qur’an na maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Ali na kiwazi kabisa akaelewa kwamba utii kwa Ali ulikuwa ni utii kwa Mtume (s.a.w.w.) na kwa Allah (Swt). Alimsikia mara kwa mara Mtume akisema: “Mwenye kumtii Ali ananitii mimi; na mwenye kunitii mimi anamtii Allah (Swt); ambaye ana uadui kwa Ali ni adui kwangu; na ambaye ana uadui kwangu ni adui kwa Allah (Swt).
Kila Mu-Iran, hata hivyo, ambaye alikwenda Madina na kusilimu, iwe wakati wa Mtume au baadae, alizitii amri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa sababu hii Khalifa wa pili akashindwa kuvumilia na akaweka vikwazo vingi juu ya Wairan. Shida hizi na taabu zilizaa uadui ndani ya nyoyo zao. Walihoji ni kwanini Khalifa awanyime haki za Uislamu kinyume na amri zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Shukurani Za Wa-Iran Juu Ya Huruma Za imam Ali.
Mbali na hali hizi, Wa-Irani walikuwa na shukurani sana kwa Ali kwa huruma zake kuhusiana na matendo waliyofanyiwa mabinti wa kifalme waliotekwa na Waarabu. Wakati wafungwa wa Mada’in (Taisfun) walipoletwa mjini Madina, Khalifa wa pili aliamuru kwamba wafungwa wote wa kike wafanywe kuwa watumwa wa Waislamu. Ali alilikataza hili na akasema kwamba mabinti wote wa kifalme ni wafungwa wa kipekee na wanapaswa wapewe heshima.
Wawili kati ya wale wafungwa walikuwa ni mabinti wa mfalme Yazdigerd wa Iran na hawakuweza kufanywa watumwa. Khalifa akauliza ni nini kifanywe. Ali akasema kwamba kila mmoja yapasa aruhusiwe kuchagua mume miongoni mwa Waislamu. Kwa ajili hiyo, Shahzanan alimchagua Muhammad ibn Abu Bakar (ambaye alilelewa na Ali), ambapo yule binti mfalme mwingine, Shahbanu alimchagua Imam Husain, mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote walikwenda kwenye nyumba za watu hawa baada kufungishwa ndoa kisheria.
Shahzanan alizaa mtoto wa kiume, Qasim Faqih, baba wa Ummi Farwa, ambaye alikuwa mama wa Imam wetu wa Sita, Ja’afar as- Sadiq. Imam Zainu’l-Abidin, Imam wetu wa nne alizaliwa na Shahbanu.
Hivi ndivyo Ushia ulivyojikita katika nyoyo za wairan

Comments