SIFA BORA ZA SHIA ZATHIBITISHWA KUTOKA KWENYE VITABU VYA KISUNNI.

SIFA BORA ZA SHIA ZATHIBITISHWA KUTOKA KWENYE VITABU VYA KISUNNI.
Katika kitabu kiitwacho Mawaddatu’l-Qurba amenukuliwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema, “Ewe Ali, Siku ya Hukumu wewe na Mashi’a wako mtakuja mbele za Allah mkiwa mmefurahi mno na kuridhia, ambapo adui yako atakuja na huzuni kubwa na mikono ikiwa imefungwa.”
Sisi Mashia ni wafuasi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Mwanzilishi wa neno Shi’a kwa maana ya “Wafuasi wa Ali” ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Kamwe hatumfuati mtu binafsi bila rejea zenye hoja za kumuunga mkono.
Hafidh Abu Hatim Razi katika kitabu chake “Az-Zainat” ambacho amekiandika kwa ajili ya kufafanua maana ya maneno fulani na Semi zinazotumika miongoni mwa Wanachuo, anasema kwamba neno la kwanza jipya ambalo lilikuja kukubaliwa na wote katika Uislamu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa ni “Shia.” Neno hili lilitumika kwa masahaba maarufu wanne: Abu Dharr Ghifar, Salman Farsi, Mikdadi bin Aswad Kindi, na Ammar Yasir. Hadith nyingi zaidi zilinukuliwa katika kuunga mkono nukta hii hii.
Sasa ni juu yenu kufikiria vipi iliwezekana kwamba wakati wa Mtume (s.a.w.w.) Wanne kati ya masahaba wake wakubwa waliitwa Shi’a. Kama Mtume (s.a.w.w.) alifikiria kuwa neno hilo ni la uzushi (bida’a), kwanini hakuwakataza watu kulitumia? Ukweli ni kwamba watu walisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) mwenyewe kwamba wafuasi (Mashi’a) wa Ali walikuwa ni wakazi wa Peponi. Walikuwa na fahari nalo na kwa uwazi wakajiita wenyewe Mashi’a.

Kuanzia siku ya kwanza mpaka leo Mashia wamekuwa wakiongoza kwa tabia nzuri za upole, usamehevu, kusaidia watu wengine na kupenda amani na utulivu kwa wanadamu wote bila kujali dini zao wala kabila. 

Comments