AMANI NA JIHADI KATIKA UISLAMU
“Amani na Jihadi” ni mada ambayo imetumiwa nje ya muktadha wa Kiislamu dhidi ya Uislamu na vyombo vya habari visivyo amini (Uislamu) vya mlengo wa kulia, wanasiasa na pia wanahistoria.
Mnamo tarehe 11, Septemba, 2001, watu wachache waliteka nyara ndege nne za kiraia na kuzitumia kama silaha kuzua hofu ndani ya Marekani, hususan kwenye yale majengo mawili ya kituo cha Biashara cha Ulimwengu (World Trade Center). Wafanyakazi wote na abiria katika ndege hizo, na vile vile takriban raia wapatao elfu tatu walipoteza maisha yao katika mashambulizi yake.
Sera za mambo ya nje za Marekani kuhusiana na nchi za Kiislamu hazithibitishi uhalali wa kwamba raia wa Marekani waliokuwa ndani ya ndege zile na yale majengo ya Kituo cha Biashara cha Dunia wauawe. Hivi sivyo Uislamu unavyofundisha. Hebu yaangalie yale maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika wakati wa vita: Yeye kwa uwazi kabisa alikataza mauaji ya wazee, watoto na wanawake.1 Wale ambao walipoteza maisha yao katika yale majumba marefu ya kituo cha Biashara cha Dunia na ndani ya ndege zile wote walikuwa ni raia, na wachache wao walikuwa ni Waislamu.
Viongozi wote wa Kiislamu ndani ya Marekani, na Duniani kote kwa uwazi kabisa walishutumu utekaji nyara ule ambao ulitendwa huko Marekani kama ni kitendo cha kigaidi ambacho hakikubaliki katika Uislam.

Shutuma hizo ziliegemea kwenye thamani ya kidunia ya utukufu wa maisha ya mwanadamu. Qur’an Tukufu inasimulia kisa cha mauaji ya kwanza katika historia, kile cha watoto wawili wa Adam (a.s.) ambamo Qabil (Cain) alimuua ndugu yake, Habil (Abel). Hili liko katika Sura ya 5 ya Qur’an Tukufu, aya ya 27 hadi 31.
1. Hurr al-‘Amili, Wasa’ilu ’sh-Shî‘a, Juz. 11, uk. 43.
2. Mwishoni mwa kisa hiki, Mwenyezi Mungu anasema: “... Yeyote atakayemuua mtu ambaye hakuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote, na mwenye kumwacha mtu hai ni kama amewaacha watu wote hai ...” (5:32)
Ni dhahiri kutokana na aya hii kwamba:
(1) isipokuwa kama mtu ameshitakiwa na kuthibitika kuwa amemuua mtu, yeye hawezi kuuawa - na
(2) kwamba kumuua mtu asiye na hatia ni sawa na kuua watu wote.
Hivyo ni Vipi Kuhusu Jihadi?
Moja ya mambo yaliyo kinyume ya zama hizi ni kwamba ingawa njia za mawasiliano zimeendelea kwa kiasi kikubwa mno, watu bado wana matatizo katika mawasiliano yenye maana ya makusudi kabisa na mazungumzo na tamaduni nyingine na dini mbali mbali. Kuna upotovu wa taarifa mwingi na kutoeleweka kwa imani ya Kiislam.

Watu wengi binafsi, wale wa kawaida na wataalam pia wamejaribu kuiunganisha tarehe 9/11 na dhana ya Jihadi katika Uislam. Katika moja ya mazungumzo ya maonyesho ya redio ya Toronto, mara baada ya Septembea kumi na moja, nilimsikia mpiga simu mmoja akasema kwamba kile kilichotokea siku ile kilikuwa kwa 10% ni ugaidi na 90% ni Uislam. Kiongozi mmoja wa kikristo mwenye siasa kali huko Marekani alisema katika onyesho lake la kwamba “Yumkini (inawezekana) Muhammad alikuwa gaidi.” Hivyo ni muhimu kuzungumza kuhusu Jihadi katika Uislam.
(a) Uislam ni Dini ya Amani Uislam kimsingi ni dini ya amani. Jina lake “Islam” linatokana na neno la kiarabu “Silm” ambalo lina maana mbili: moja ni “kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu” na ya pili ni “amani.” Maana zote zinaingiliana.
Wakati wowote Waislam wanapokutana, wanatumia maamkizi ya amani: “as-salamu alaykum - amani iwe juu yako,” na huyo mtu mwingine anajibu kwa kusema “alaykumus-salam - juu yako iwe amani.”
Sala za kila siku zinaanza na kumsifu Allah kama “Rehema na Mwenye fadhila” na zinaishia na salam za amani kwa wote.
(b) Dhana ya Jihadi inahitaji kueleweka vizuri. Watu wengi katika vyombo vya habari wanayachukulia maneno ya Qur’an nje ya muktadha wake. Na kwa hiyo hebu tuone ni nini maana ya Jihadi?
Hili neno “Jihad” halina maana ya “vita takatifu.” Huu ni utoaji wa ki-magharibi wa dhana pana katika mafundisho ya Kiislam. Muulize mtaalam yoyote yule wa lugha ya kiarabu na atakwambia kwamba “Jihad” haina maana ya “vita takatifu.” Maneno, au usemi huu wa “vita takatifu” umekuja kutokana na dhana ya Kikristo ya “vita ya haki (crusade – vita vya msalaba),” na umetumika hovyo hovyo kama lahaja ya Kiislam tangu zile siku za Krusedi.

Hivyo basi, Jihadi ina maana gani? Katika lugha ya kiarabu, neno Jihadi kwa maana halisi ni kujitahidi na kufanya kazi kwa bidii sana kwenye jambo fulani. Katika Istilahi za Kiislam, linabakia na maana halisi hizo katika vipimo viwili tofauti, ambavyo vinaelezewa kwa “Jihadi kubwa” na “Jihadi ndogo.”
Jihadi kubwa inajulikana kama mashindano ya kiroho, mashindano kati ya nguvu mbili ndani yetu: nafsi na mwili. Moyo unapambana na matamanio ya kimwili. Mapambano haya ya kiroho ni Jihadi inayoendelea ndani ya kila mmoja wetu. Uislamu unawatarajia wafuasi wake kutoa kipaumbele kwenye nafsi na dhamira juu ya mwili na tamaa zake.
Kule kufunga katika mwezi wa Ramadhani ni mfano wa mafunzo ya kila mwaka kwa ajili ya Jihadi hii.
Comments
Post a Comment