FADAK

FADAK
Fadak ni shamba lilokuwa kaskazini ya Madina, umbali wa safari ya siku 2 au 3, ilikuwa ni ardhi yenye rutuba sana, kwa mujibu wa Ibn Abi Hadid, vijisitu vya tende havikuwa vidogo kama vile vya Kufa ambazo pato lake lilikuwa kati ya 24,000 dinar. Ilikuwa inakaliwa na kabila la Mayahudi.

Katika mwaka wa 7 A.H., Mtume alipigana vita dhidi ya Mayahudi wa Khaibar, kwa sababu walivunja mkataba na Waislamu. Baadhi ya ngome zao zilichukuliwa; mbili au tatu zilizingirwa. Mwishowe  walipendekeza mpango ambao maisha yao, dini, heshima yao nk. itakuwa salama, na wataondoka katika ngome na kufanya  kazi za shamba kwa ajili ya Waislamu. Mapatano yalifikiwa;  Mayahudi waliruhusiwa kufanya kazi kwenye mashamba kwa niaba ya Waislamu na mazao yaligawanywa kati ya Mayahudi na Waisalmu nusu kwa nusu.

Kwa mujibu wa aya ya Qur’an (8:41) moja ya tano ya ngome na ardhi alipewa Mtume kama Khums, na nne ya tano iliyobakia ilikwenda kwa Waislamu.
Wakati Mayahudi wa Fadak waliposikia vita ya Khaibar na matokeo ya makubaliano, walianza kufikiria kuhusu wao wenyewe. Wakati huo huo akaja mjumbe kutoka Madina, akawalingania Uislamu.  Walikataa kukubali Uislamu, lakini kwa matakwa yao wenyewe,  walikubali amani kwa masharti yafuatayo:
a. Watatoa nusu ya ardhi yao kwa Mtume, nusu iliyobaki iwe  kwenye miliki yao.
b. Watafanya kazi katika ardhi ya Mtume na kugawana mazao yake.
c. Mtume atakuwa na mamlaka ya kuwafukuza kutoka Fadak wakati wowote atakao, lakini itampasa kuwalipa malipo kamili ya mgao wao wa ardhi na mali yao.
Mtume alikubali masharti yao3.
Baadhi ya Waislamu walifikiri kwamba Fadak ilikuwa vile vile mali ya Waislamu kama Khaibar.  Lakini ni kutokuelewa kwao, kwa sababu zamani kabla ya hilo, katika  suala la Banu Nazir, sheria ilitangazwa rasmi kwamba chochote  kinachokuja kwa Mtume bila ya kupigana vita, kitakuwa ni mali  binafsi ya Mtume, kwa ajili ya matumizi yake au kugawa kwa  atakaeona inafaa, na Qur’an inasema:
“Na mali aliyoleta Allah kwa Mtume Wake hamkuyakimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Allah huwapa mamlaka Mitume Wake juu ya wowote awatakao, na Allah ana uwezo juu ya kila kitu.” (59:6)
Banu Nazir walifukuzwa kutoka Madina mwanzoni mwa mwaka  wa tatu hijiriyya. Waliruhusiwa kuchukuwa chochote kile  kinachowezwa kubebwa na ngamia wao isipokuwa silaha.

Katika kuwasili kwake Madina, Mtume alifanya uhusiano wa  kindugu, akimfanya Muhajir ndugu wa Ansar na kila Ansar aligawa mali yake yote nusu kwa nusu na ndugu yake Muhajir, kiasi kwamba  kama mirathi ya Ansar ilikuwa ikigawanya miongoni mwa kaka  na dada zake, ndugu Muhajir alijumuishwa ndani yake.

Abu Bakar alifanywa ndugu na Kharijah bin Zayd; ‘Umar na ‘Utban bin Malik Ansari walifanywa ndugu, kama walivyofanywa ‘Uthman na Aws bin Thabit Ansar, na kadhalika Ali peke yake aliachwa nje ya undugu huu, Mtume alitangaza kwamba Ali ni ndugu wa Mtume mwenyewe.

Alipopata mali ya Banu Nazir, Mtume kwa matakwa yake mwenyewe  aliamua kuigawa miongoni mwa Muhajirin na akawaondolea  Ansar mzigo huu. Alifanya hivyo, na akawajumuisha katika orodha hii Ansar wawili masikini sana - Abu Dajjanah na Sahl ibn Haneef.
Hivyo Muhajirin wote, wakiwemo Abu Bakar, ‘Umar na ‘Uthmani walipata mgao wao kutoka kwenye ardhi hiyo na ikawa mali yao  binafsi. Haikuwa kwa ajili ya “kujikimu” tu.
Katika njia hiyo hiyo Fadak ikawa mali ya binafsi ya Mtume na  aliisimamia yeye mwenyewe.7
Kisha aya nyingine ya Qur’an ilikuja: “Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake....”  (17:26)
Mtume alimuuliza Jibril maana ya aya hii. Akasema: “Mpe Fatimah  Fadak; itakuwa ni chanzo chake cha mapato na watoto wake.”8 Mtume akampa Fatimah Fadak; na alikuwa akiitumia kama mali yake mwenyewe; wakala wake alikuwa kule akiangalia maslahi yake. Hii iliendelea mpaka Mtume alopofariki na Abu Bakar akachukuwa  umiliki wa Fadaka kwa nguvu.

Fatimah alipinga dhidi ya uporaji huu wa mali yake,  akisema kwamba Mtume alimpa yeye. Abu Bakar akamuambia  alete mashahidi kuthibitisha jambo hili.
Sasa Fatimah alikuwa tayari katika umilki wa mali hii; na kwa  mujibu wa kanuni za ki-Islamu, umiliki wenyewe ni uthibitisho wa kutosha wa umilikaji. Kama Abu Bakar alidai mali ile kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya taifa la ki-Islamu, basi ni yeye, kama mdai ambaye alipaswa kuleta mashahidi kuunga mkono madai yake. Lakini aliweka dhima ya kuthibitisha juu ya Fatimah, akipuuza  Sheria ya ki-Islamu.

Huu ni uthibitisho wa dhuluma walizofanyiwa Ahlulbayt wa Mtume kutokana ubabe wa watawala waliojiita wenyewe kuwa ni makhalifa wa Mtume. Ukweli ni kuwa Mtume hawezi kumpa ukhalifa mtu anayedhulumu mali za watu tena alianzia dhulma kwa kuwadhulumu wanafamilia wa Mtume.

Rejea
3. Yaqut Al-Hamawi, Mu’jamul-Buldan; Ibn Abil Hadid, Sharh Nahjul Balaghah     j.16 uk.210; al-Tabari, Annals, J. Uk. ; Ibnul Athir, Tarikhul Kamil.
6 Tafsir Ad-Durr’l-Manthur, j.6 uk.187-190 7 Ar-Razi, Tafsir Kabir, Az-Zamakhshari, Tafsir Al-Kashshaf

8 Suyuti, Ad-Durrul-Manthur, j.4, uk.177; Suyuti, Lubabun-Naqul, imechapishwa   katika pambizo laTafsir al-Jalalain, j.2, uk.19. 

Comments