FAMILIA
KATIKA UISLAMU
Familia
katika Uislamu, ina utaratibu mzuri na wa hali ya juu sana, na ni utaratibu
unaoheshimiwa sana na ni mahali panapostahiwa. Ni kwa sababu hii na ndio maana
Uislamu huipa nguvu (familia).
Ndoa
ndio mwanzo wa kuunda familia na kisha jamii, na uangalifu wa Uislamu katika
nguzo hiyo muhimu, hatimaye unaongoza kuelekea katika maisha ya amani na
furaha.
Qur’an
(60:11) imendikwa: Enyi mlioamini,
watakapo- wafikieni wanawake waaminio wanaohama, basi wajaribuni, Mwenyezi
Mungu ndiye Ajuaye zaidi imani yao, kama mkijua kuwa wao ni waaminio basi msiwarudishe kwa makafiri. (Wanawake) hawa si halali kwao,
wala wao (wanaume makafiri) si halali kwao; na warudishieni waume zao mali
walizotoa. Wala kwenu si hatia kuwaoa
ikiwa mtawapa mahari yao; wala msiwaoe wanawake makafiri, na ombeni
mliyoyatoa, nao waombe walivyovitoa. Basi hii ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu
Anayowa- hukumu kati yenu; na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye, Mwenye hekima.
Hii
ni miongoni mwa aya nyingi zinazofafanua kuwa waislamu tunatakiwa kuwaoa
wanawake wema na waislamu. Kuna athari kubwa endapo kama mtu ataoa au ataolewa
na mtu asiyekuwa mwislamu au mtu anayedai kuwa ni mwislamu lakini hafuati
maadili ya kiislamu. Maisha yao ya kiroho yatakumbwa na vikwazo vingi na malezi
ya watoto yatakuwa magumu kabisa maana kila mmoja atakuwa anajitahidi kuvutia
watoto upande wake, hatimaye watoto wataharibika.
Taasisi
hii muhimu ya familia inatakiwa iundwe kwa umakini na pia isimamiwe kwa umakini
kwa kuwalea watoto vizuri kwa kuwasomesha elimu zote, lakini elimu ya awali
ihusiane na kumpenda Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlulbayt
wake. Mtoto aliyelelewa kwa misingi hii tunaamini kuwa atakuwa mwema.
Comments
Post a Comment