JE IBILISI NI MALAIKA
AU JINI AU NANI HASA?
Qur'an imeandikwa; Na
Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adamu! Wakasujudu ila Iblis, akakataa na
alikuwa miongoni mwa makafiri (2:34).
Ibilis hakuwa Malaika;
maana Mwenyezi Mungu anasema, Malaika 'hawamwasi Mwenyezi Mungu Aliyowaamuru,
na hutenda wanayoamrishwa" (66:7); lakini Ibilisi aliasi, hivyo hakuwa
Malaika.
Katika Aya hii
Mwenyezi Mungu amefupisha maneno na inaonekana Ibilisi kana kwamba alikuwa
mmoja wa Malaika. Lakini katika sura 7:13 Mwenyezi Mungu anaonyesha kuwa
Ibilisi pia alipewa amri ya kumtumikia Adamu lakini hakutii, ndipo Mwenyezi
Mungu akamkasirikia.
Sura 18:51 inaeleza
kuwa Ibilisi alikuwa miongoni mwa jinn (viumbe wa siri) ambao, kinyume na
Malaika, wao walipewa uwezo wa kutii na kuasi.
Iblisi ni jini
lililokuwa linaishi na malaika kwa muda mrefu na ilipotolewa amri ya kumtii
adamu yeye pekee ndiye aliyegoma na hivyo kulaaniwa na Allah na kufukuzwa toka
katika neema za Allah. Iblisi alimwomba Mwenyezi Mungu ampe muda mrefu ili
aweze kumpotosha Adam na watoto wake. Mwenyezi Mungu akampa ruhusa hiyo. Kuanzia
siku ile mpaka leo anaendelea na kazi yake ya kuhakikisha kuwa watu
hatumtumikii Allah ipasavyo na hivyo twende Jahannam pamoja naye.
Allah ameahidi kuwa
hatoruhusu Ibilis awapotoshe watu wacha Mungu, lakini wale wataoafikiana na
shetani (ibilis) wakusanywa pamoja na kujazwa ndani ya Moto wa Jahannam siku
ile ya hukumu.
Tunamwomba Allah atulinde
kutokana na upotoshaji wa Shetani (ibilisi) na majeshi yake.
Comments
Post a Comment