JESHI LA USAMA BIN ZAID
Katika mwaka wa kumi Hijjra, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipeleka jeshi kwenda kupigana Roma. Katika jeshi hilo Mtume aliamuru liongozwe na Usama bin Zaid akasema:- "Nenda ukapigane alikouliwa baba yako".
Katika mwaka wa kumi Hijjra, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipeleka jeshi kwenda kupigana Roma. Katika jeshi hilo Mtume aliamuru liongozwe na Usama bin Zaid akasema:- "Nenda ukapigane alikouliwa baba yako".
Uteuzi huu Masahaba haukuwapendeza, kwa hiyo
walisikika wakipinga amri hiyo wakisema: "Itakuwaje mtoto mdogo huyu apewe
madaraka makubwa juu yetu? Miongoni mwa waliopinga ni Abubakar nisidiq na Umar
bin Khatab.
Ilipomfikia habari hii Mtume (s.a.w.) aliwaambia:
"Nimesikia lawama zenu nilivyomtawalisha Usama katika jeshi hili, sioni
ajabu, maana mlikwisha nilaumu zamani nilipomtawalisha baba yake kabla yake.
Wallahi baba yake alikuwa ni mtu aliyefaa kushika uongozi wa jeshi hilo, kama
ambavyo mtoto huyu anastahiki kabisa uongozi wa jeshi hili". Mtume (s.a.w.)
akasisitiza watu wote isipokuwa Ali, waende na jeshi Ia Usama akisema:
"Andaeni jeshi la Usama, Mwenyezi Mungu amlaani atakaebaki asiende na
jeshi hilo".
Tazama: AI-miIalu Wannihal Juzu ya 1 Ukurasa wa 20.
Alipofika nje
kidogo ya mji, Usama aliweka kambi ili watu wakusanyike pamoja tayari kwa msafara.
Hapo Abubakar akaanza kumshawishi Usama kwamba asipeleke hilo jeshi kwa sababu
haiwezekani kutoka na kumwacha Mtume (s.a.w.) akiwa hali hii ya maradhi.
Abubakar alikuwa ni mtu mzima kwa umri kuliko Usama, takriban umri wa Abubakar wakati
huo si chini ya miaka hamsini, na umri wa Usama si zaidi ya miaka Kumi na Tisa.
Abubakar alitumia hila mbali mbali kwa kuendesha majadiliano kati yake na kijana mdogo Usama, baina ya jeshi liende kupigana Roma kama alivyoamuru Mtume, au lisiende kama anavyotaka Abubakar.
Abubakar alitumia hila mbali mbali kwa kuendesha majadiliano kati yake na kijana mdogo Usama, baina ya jeshi liende kupigana Roma kama alivyoamuru Mtume, au lisiende kama anavyotaka Abubakar.
Hali hii ilichelewesha na kuchukua muda mrefu bila ya
kwenda alikoamrisha Mtume, mpaka mauti yakamfikia akafa Mtume (s.a.w.).
Mwenyezi Mungu anasema: "Haiwi kwa mwanamume
aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake
wanapohukumu jambo lo lote wawe na khiari katika hukumu hiyo. Na mwenye kumuasi
Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi" (33:36).
Amri aliyohukumu Mtume hapa ni Usama kuwa Mkuu wa jeshi litakalokwenda kupigana
Roma, matokeo ni kwamba; baadhi ya Waislamu hawakutii amri hiyo. Katika Aya,
iliposema: "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika
amepotea upotevu ulio wazi." Hapa Abubakr na Umar wanapatikana na hatia ya
kumuasi Mtume (s.a.w.), na mwenye kumuasi Mtume amemuasi Mwenyezi Mungu.
Kama viongozi hao walikuwa waasi kiasi hiki, itakuwaje
kwa wafuasi wao?
Comments
Post a Comment