KHALIFA
AU IMAMU WA TATU WA WAISLAMU
Naye ni Hussein bin Ali bin Abi Talib (a.s.), na mama yake ni Bibi
Fatima, binti yake Mtume (s.aw.w.), na yeye ni mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), ni wa
tatu katika Makhalifa, na ni baba wa maimamu tisa baada yake, na ni Imam wa
watu baada ya kaka yake (Imam Hassan) (a.s.).
Kazaliwa katika Madina Munawwara, mwezi tatu Shaaban, mwaka wa nne
wa Hijiria.
Kauwawa hali ya kudhulumiwa kwa upanga katika hali ya kiu, katika
mapigano ya Ashura [6] yaliyoko mashuhuri, siku ya Ijumaa, mwezi kumi mfungo nne mwaka wa
sitini na moja wa Hijiria, na akasimamia mambo ya mazishi yake baada ya siku
tatu mtoto wake Ali Zainul Abediin (a.s.), akamzika mahala lilipo kaburi lake
sasa katika mji wa Karbala Mtakatifu.
Fadhila zake hazitajiki. Yeye ni manukato ya Mtume (s.a.w.w.),
kama alivyo sema Mtume (s.a.w.w) kwa yeye na kwa kaka yake Imam Hassan (a.s):
"Wao ni manukato yangu duniani".
Na akasema Mtume (s.aw.w.): "Hussein ni katika mimi na mimi
ni katika Hussein." Pia akasema: "Hassan na Hussein ni maimamu ijapokuwa
wamesimama au wamekaa."
Alikuwa mwenye elimu kubwa na mwabudu mno, alikuwa anasali kila
usiku elfu rakaa kama baba yake Amirul muuminiin Ali (a.s).
Alikuwa anabeba siku nyingi mifuko ya vyakula kuwapelekea
mafakiri, mpaka ikaonekana alama ya mizigo baada ya kuuwawa kwake; na alikuwa
mkarimu, mpole na alikuwa anaghadhibika anapoona mtu akifanya kinyume cha
sheria ya kiislamu.
Na katika ukarimu wake, ni kuwa Mwarabu mmoja alimkusudia kwa
kutaka haja yake. Akamfanyia mashairi (nashidi), akasema:-
"Hakurudi utupu ambaye akakutumai na akakusudia mlangoni
kwako."
"Wewe ni mkarimu na wewe mwenye kutegemewa: baba yako alikuwa
muuwaji wa fasiki (wale wanaomwasi Mwenyezi Mungu)."
"Lau si ambayo yamekuwa kutoka kwa wazee wenu, ungalitufunika
moto wa Jahannam."
Imam Hussein (a.s.) aliposikia nashid hii akampa dinari elfu nne,
na pia akamtaka msamaha kwa mashairi haya:-
"Chukua hizi, mimi kwako ninataka msamaha, jua kuwa mimi ni
mwenye huruma kwako.
"Lau tungalikuwa na fimbo katika mwenendo wetu wa mapema
yangalikuwa mawingu yetu juu yako yenye kunywesha (kama ungalikuwa utawala wa
dola ya Islamu mkononi mwetu, tungalikusaidia zaidi).
"Lakini khadaa ya zama ina migeuzo, na kitanga changu ni
kichache cha nafaka (matumizi)."
Akaishia (a.s.) kwa msimamo wake wa ushujaa (ambao hapana mfano
ulimwenguni) sharia za Ki-Islamu na dini ya baba yake Rasulullah (s.a.w.w),
kamwe kuhuisha ulimwengu mzima mpaka siku ya kiyama.
Yeye ni bwana wa mashahidi na mbora mno baada ya kakaye.
Comments
Post a Comment