KHALIFA
WA MTUME AU IMAMU WA NNE WA WAISLAMU
Naye ni Imam Ali bin Hussein (a.s.), na mama yake ni Shah Zanan,
binti ya Mfalme Yazdajurd. (ShahZanan-Malkia wa wanawake). Bibi huyo tena
anaitwa "Shahr Bano" (Bibi wa Mji).
Imam huyu kazaliwa Madina Munnawwara, nusu ya mwezi wa mfungo
nane, mwaka thelathini na sita, siku aliyoteka Ali (a.s.) Basra. Na kafa hali
ya kupewa sumu siku ya Jumamosi, mwezi ishirini na tano, mfungo nne, mwaka wa
tisini na tano wa Hijiria. Na umri wake mtukufu ni miaka khamsin na saba.
Kazikwa Bakii, mji wa Madina.
Alikuwa bila ya mfano katika elimu, na ibada na fadhila, na
uchamungu, na kuwasaidia waliopata shida. Na wamepokea kutoka kwake (a.s.)
wanachuoni wengi, na yamehifadhiwa kutokana kwake mawaidha, na uradi na
Historia na mengineyo.
Alikuwa anatoka usiku anachukua mifuko ndani yake zimo dinari na
dirhamu; na wakati mwingine akibeba vyakula au kuni, hata akifika majumba
ya masikini na hugonga mlango, kisha huwapa alichonacho. Alikuwa akiuficha uso
wake kwa sababu wasimjue masikini. Zama alipokufa ndipo walimjua kuwa yeye
ndiye mchukuaji mifuko ya mapesa na vyakula.
Alikuwa anapendeza mno kula nao masikini na viwete na mayatima.
Alikuwa mzuri mno wa tabia, Alikuwa anasema anapomjia mtu kutaka msaada:
"Marahaba kwa mwenye kufikisha akiba yangu akhera."
Na katika uchamungu wake, alikuwa anasali mchana na usiku rakaa
elfu moja; na utapoingia wakati wa sala hutetemeka mwili wake, na hugeuka uso
wake rangi ya njano, na kiwiliwili chake hutetemeka kama kuti. Na alikuwa
anaitwa "DHUTH-THAFANATI" yaani mwenye magome. Na sababu yake kuwa
kwa wingi wa kusujudu yakamtokea magome katika paji la uso, na vitanga vya
mikono na magotini na katika vidole gumba. Kila miezi sita yakikatwa magome
haya.
Na alikuwa kila anapomkumbuka Mwenyezi Mungu na neema zake,
husujudu, na kila anaposoma aya yenye sijida, husujudu, na kila anapomaliza
swala ya faradhi husujudu na huitwa As-Sajaad (yaani mwenye kusujudu sana).
Na wakati ule walikuwa wakisema "Hatukumwona Mquraish mbora
kuliko yeye."
Na alitukanwa na mtu katika jamaa zake na kusikia yasiyompendeza,
naye alikaa kimya. Baada ya muda mdogo akaenda Imam (a.s.) kwake. Wakadhani
waliokuwepo kuwa Imam (a.s.) anataka akamrudishie, sivyo, laa hasha, alisoma
Imam (a.s.) maneno ya Qur-an haya: "WAL KADHWIMINAL GHAIDHY WAL AAFINA
ANINNASI WALLAHU YUHIBUL MUHSINIIN" (Na wavunjao ghadhabu na wanaosamehe
watu, na Mungu anawapenda watendao mema). Kisha Imam (a.s) akasema kwa yule
mwenye kutukana: "Ee ndugu yangu! wewe umetushambulia sasa hivi, ukasema
uliyoyasema, ikiwa ndivyo ulvyo sema kwangu, basi Mungu anisamehe, na ikiwa
ulivyosema sivyo basi Mungu akusamehe."
Wakati sisi waislamu wa kweli tukimsifu imam wetu wanne, mawahhabi
wao wanamsifu khalifa wao na muuaji mkuu wa waislamu naye si mwingine ni Yazid
bin Muawiyyah (alayhi hawia)
Comments
Post a Comment