KIFO CHA BI FATUMA BINT RASULULLAH (A.S)
Baada ya uislamu kukamilika kwa kutangazwa imam Ally kuwa
khalifa wa kwanza kuongoza Uislam pindi tu Mtume atakapofariki, mtangazaji
akiwa ni Mtume Muhammad (s.a.w.w) muda mfupi baada ya hija walipofika eneo la
Ghadeer Khum mnamo tarehe 18 Dhulhija mwaka wa 10 Hijria. Hapo Mtume alitangaza
bayana kuwa yeyote yule anayeamini kuwa yeye Mtume ni kiongozi wake na Ally pia
ni kiongozi wake, kisha lilijengwa hema na Masahaba wakaagizwa watoe mkono wa
utii (baia) kwa imam Allh (a.s).
Mtume aliporejea tu Madina alianza kuugua, binti yake Fatuma,
Imam Ally na wajukuu zake yaani Imam Hassan, Imam Hussein, bi Zainabu na Ummu
Kulthum walikuwa mstari wa mbele katika kumuuguza.
Siku moja Mtume alimwambia binti yake kuwa anakaribia kufa na
kwamba Fatuma atamfuatia mara moja kutokana na hujuma na mateso atakayo yapata
toka kwa baadhi ya Masahaba wake.
Abdallah bin Abasi (r.a) anahadithia kuwa wakati Mtume
alipokaribia kufa, alilia sana kiasi cha kulowesha ndevu zake zote kwa machozi.
Alipoulizwa analilia nini, Mtume alijibu ninalilia kizazi (Ahlulbayt) changu,
kutokana na dhuluma na mateso watakayofanyiwa na baadhi ya masahaba wake pindi
tu atakapofariki dunia. (Buharul Anwar Juzu ya kumi).
Mtume alifariki pindi alipokuwa anazungumza na familia yake
niliyoitaja hapo juu. Familia nzima ilihuzunika sana na kulia kweli kweli.
Waislamu walikusanyika msibani (msikitini) lakini wakamkuta
Omar bin Khatab ambaye aliwatisha kwa kuwaambia kuwa Mtume hakufa na hatokufa
mpaka wanafiki waishe, yeyote atakayesema kuwa Mtume kafa atamchinja mara moja.
Waislamu wakatawanyika na kurudi makwao.
Hapo ndipo baadhi ya masahaba wapenda madaraka
walipokusanyika katika ukumbi wa Saqifa Bani Sa’dah kuchaguana ili kumpindua
imam Ally toka kwenye cheo chake cha ukhalifa. Kwa kulazimishwa na Omar bin
Khatab kwa kutishiwa kuchinjwa, hatimaye rafiki yake yaani Abubakar akapewa
ukhalifa.
Habari hizi zilimfikia Fatuma ambapo alishituka sana kutokana
na mapinduzi hayo na akajaribu kuwashawishi watu wamuunge mkono yeye pamoja na
mme wake. Lakini watu wengi walimkatalia wakiogopa kuuawa na Umar bin Khatab. Fatuma
alilia sana mpaka Imam Ally alimjengea nyumba maalumu (bait ul Huzn) ili aweze
kupata faragha anapoomboleza kifo cha baba yake na pia akumbukapo dhulma za
Masahaba dhidi ya Ahlulbayt.
Baada ya kunyakua madaraka, Abubakar alifanya dhulma yake ya
kwanza kwa kutangaza kuwa mitume hawarithiwi na kwamba mali waziachazo ni za
waislamu wote. Hii ni kinyume na Qur’an inayobainisha kuwa kila mtu anarithiwa
na warithi wake na pia Qur’an inathibitisha kuwa hata mitume wanarithiwa pale
ambapo imeandikwa kuwa Seleman alimrithi baba yake Daudi. Kila mwislamu anajua
kuwa Daudi ni Mtume na Selemani pia ni Mtume. Kama Daudi alirithiwa kwa nini
Mtume asirithiwe na mtoto wake wa pekee. Lakini ni kinyume na Uislamu mkwe
kupora mirathi ya mjukuu wake hata kama hakuzaliwa na binti yake.
Ni siku hiyo hiyo ndipo Abubakar aliagiza jeshi lake likiwa
chini ya Umar bin Khatab kwenda kuwakusanya waislamu kwa lazima na
kuwalazimisha watoe mkono wa utii kwake. Kazi hii ya kuwalazimisha watu ilifika
mpaka kwa Imam Ally (a.s) ambapo walifanya vitisho kwa siku kadhaa, hatimaye
Umar alikwenda kumalizia kazi pale alipokwenda ni moto na kuinguza nyumba ya
Ally na bi Fatumah ambapo bi Fatuma alijeruhiwa na majaraha hayo ndiyo
yaliyopelekea kifo chake miezi miwili tu baada ya kifo cha baba yake.
Innalillahi wainna
ilayhi rajiuun.
Tunamwomba Allah awalaani wote walioshiriki kumdhulumu bibi
huyu Mtukufu.
Comments
Post a Comment