MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {3}

MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {3}

{1}Ukarimu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Yule anayetoa {zaka, Sadaka na mengineyo} na kumcha {Mwenyezi Mungu} na kusadiki mambo mema {akafanya}, Tutamrahisishia njia ya kwenda peponi. {Qur'an Sura ya 92 aya ya 6-7}. Mtume {s.a.w.w.} amesema "Mkarimu ni mpenzi wa Mungu na bahili adui wa Mungu".

{2}Utawa:
{Uzuilifu wa tamaa hasa wa kike na kiume} Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Mwenye kuzuwia tumbo lake na haramu, na utupu wake kwa haramu na ulimi wake na kila kilicho katazwa kusema, basi mtu huyo amejilinda kikweli kweli na mahala pake ni peponi.

{3}Kuwasaidia wanyonge:
Mwenyezi Mungu amesema:"{Wamchao Mwenyezi Mungu ni ambao} katika mali zao ni haki ya {masikini} aombaye na ujizuiaye kuomba." {Qur'an, Sura ya 51 aya ya 19}

Comments